Haya ni Makaburi Yaliyopo Katika Mji wa La Noria, Chile. Roho za Wafu Bado Zinaishi Hadi Sasa, Usiku Huonekana Watu Wakienda Kusoma Katika Shule Iliyopo Jirani. Makaburi Huonekana Yapo Wazi. Watu Wote Walihama, Shule Zote Zilitelekezwa. Ni Hatari Kupita Huko.
Moja ya stori zinazosimuliwa sana kila uchwao katika mji wa La Noria magharibi mwa Chile ni kuhusu kutisha kwa makaburi ya La Noria hadi kupelekea kutengwa na makazi au hata huduma za kijamii zilizokuwa karibu na eneo la makaburi hayo.
Zamani tangu mwaka 1826 mji huu ulikuwa unasifika kuwa na migodi ya madini na shughuli nyingi za kilimo, baadae moja ya eneo la mji likategwa na kuwa eneo la kuzikia, lakini kilichofuata baada ya hapo ni historia.
Makaburi yalianza kutisha, mashuhuda wanadai usiku wanashuhudia watu kama wanafunzi wakitoka makaburini humo na kwenda katika madarasa ya shule iliyokuwa karibu, wengine walidai wanashuhudia makaburi yanakua tofauti kila siku kama vile kuna shughuli hufanyika hapo.
Miaka michache nyuma vyombo vya habari vilifanya uchunguzi katika makaburi hayo kuujua ukweli, inaelezwa walibaini kuwa nyakati za usiku makaburi yanaonekana kuwa wazi na mchana yanakua kawaida, haikujulikana sababu.
Wakazi wote katika maeneo ya karibu wakahama, na hata huduma nyingine za kijamii kama shule zilitelekwezwa
kutokana na mambo hayo ya kutisha, yamebaki magofu tuu.
Sababu inayoelezwa kupelekea makaburi hayo kutisha ni kutokana na miaka hiyo mji huu kuwa na shughuli nyingi kama kilimo na uchimbaji madini, hivyo kupelekea watu wengi kufanywa watumwa kwa kutumikishwa kazi, wengi walikufa wakiwemo akina mama na watoto, inadhaniwa labda roho zao ndio hizo zilizopo hadi leo.
Ukipita hapo utakutana na mabaki ya majeneza yakiwa wazi, mifupa ya binadamu imetapakaa kila mahali, wenyeji wanasema inawezekana roho hizo zilikasirika kutokana na uonezi zilizowahi kuupitia.
.webp)

Maoni