FAIDA ZA HILIKI MWILINI MWAKO

JE WAZIJUWA FAIDA ZINAZO PATIKANA KWA KUTUMIA MBEGU ZA HILIKI KIAFYA MWILINI MWAKO?


FAIDA ZA HILIKI MWILINI MWAKO ZIFUATAZO NI BAADHI YA FAIDA ZA HILIKI KIAFYA





1. Kuondoa harufu mbaya katika kinywa

Hiliki ina viashiria ambayo vinaweza kuuwa vijidudu vinavyosababisha harufu mbaya katika kinywa.

Tafuna hiliki kila baada ya mlo ili kuacha kinywa chako kikiwa fresh na harufu nzuri.

Sukutua kinywa chako kwa maji ya vuguvugu ya hiliki mara mbili kwa siku,ili kuondoa tatizo la harufu katika kinywa


2. Hiliki Inahimarisha afya ya mfumo wa kusaga na kusharabu chakula na pia inachochea uzalishaji wa nyongo kwa ajili ya kuyeyusha vyakula vyenye mafuta mengi mwilini hii usaidia kupunguza gas tumboni, kuondoa  kiungulia na kutibu maumivu ya tumbo

Pendelea kutia hiriki katika vyakula au kunywa sana chai ya hiliki kuhimarisha usagaji wa chakula


3. Hiliki inasaidia kuleta hamu ya kula:-

Kutokana uzalishaji wa nyongo kwa ajili ya kunyeyusha vyakula vya mafuta na virutubisho vingine pamoja na kuondoa gas vitu ambavyo vinachangia kuondoa hamu ya kula

Tia unga wa hiliki katika supu au tafuta mbegu zake ili kurudisha hamu ya kula


4. Hiliki inasaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mapafu na kuzibua mirija ya hewa hivyo kuwapa unafuu wenye matatizo ya pumu, na matatizo mengine ya upumuaji

Tumia hiliki kwa kutafuna kwa kiasi au kwa kunywa kusaidia matatizo ya pumu Kama vike kifua kubana na kukohoa.


5. Hiliki inaondoa maumivu ya kichwa yanayotokana na tatizo la usagaji wa chakula.

Kunywa kikombe kimoja cha chai ya hiriki kuondoa maumivu ya kichwa.




Maoni