Je, wazijua ajira/ kazi 10 za siku zijazo ni zipi?

Je, wazijua ajira10 za siku zijazo ni zipi?

Mwanamke mwenye furaha

Chanzo cha picha,asmoh online

Ajira ambazo zitahitajika zaidi katika siku zijazo huenda tayari zimebainika.

Licha ya hofu kwamba kukua kwa kiteknolojia kutamaliza sehemu kubwa ya kazi, wataalam wanakadiria kasi kubwa ya kuibuka kwa nafasi mpya za kazi.

"Sote tumeshuhudia kinachoendelea kwa kutumia akili bandia na jinsi teknolojia hiyo inavyokuwa kwa haraka katika tasnia mbalimbali," alisema Saadia Zahidi, mkurugenzi mtendaji wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) na mkuu wa Kituo cha Uchumi Mpya na Jamii ya Jumuiya ya Mashirika ya Kimataifa.

Ingawa fani mbili zinazoibuka na ambazo zinakadiwa kukuwa kwa kasi ya juu zaidi katika miaka mitano ijayo ni ya wataalamu wa akili bandia na wataalam wa kujifunza mashine, kulingana na WEF, kuna fursa zingine za kazi ambazo pia zinatarajiwa kujitokeza.

Kwa mfano, ajira ya wataalam katika sekta uendelevu ya mazingira au waendeshaji wa zana za kilimo, ni baadhi ya kazi 10 bora ambazo zitakuwa na mahitaji makubwa zaidi katika miaka mitano ijayo.

tt

Chanzo cha picha,asmoh online

Makadirio haya yalifanywa na shirika lenye makao yake makuu Uswizi, kulingana na uchunguzi wa kina wa makampuni makubwa 803 ambayo yanaajiri zaidi ya watu milioni 11 katika chumi 45 za maeneo tofauti ya dunia.

Utafiti huo ulionyesha kuwa karibu asilimi 75 ya makampuni yaliyohojiwa yanaamini kwamba yatatumia teknolojia ya akili bandia katika biashara zao.

Na kuhusu athari za kiteknolojia katika ajira, waajiri wa makampuni makubwa wanakadiria kuwa ajira nyingi zaidi zitaibuka kuliko zitakazopotea katika miaka mitano ijayo.

Hizi ndizo kazi 10 zilizo na uwezekano wa juu zaidi wa kukua kati ya 2023 na 2027, kulingana na utafiti wa WEF.

1. Mtaalamu wa akili bandia na mtaalam wa kujifunza mashine

Kazi hii inalenga kufanya kompyuta kuiga mawazo ya binadamu.

Wataalamu wa akili bandia wanatarajiwa kuunda mifumo ya kompyuta inayoweza kufikiria kama watu na kutatua matatizo magumu.

Kazi hii pia inalenga zaidi kuwezesha mfumo wa akili wa bandia kuwa na uwezo wa kutatua shida, kujibu maswali na kukamilisha kazi ambazo kawaida hufanywa na wanadamu.

Kompyuta

Chanzo cha picha,asmoh online

Kwa hivyo, mfumo lazima uweze kufanya kazi kwa uhuru kamili, kama akili inayojitegemea ambayo inaweza kutolewa kwa seti mbalimbali za data ili kuchanganua na kupata hitimisho lake.

Badala yake, mtaalamu wa kujifunza kwa mashine husaidia mifumo ya akili bandia kutatua tatizo fulani kwa ubora zaidi.

Ingawa mwanasayansi wa AI anafanya kazi kuunda akili huru inayoweza kutatua matatizo mengi, mtaalamu wa kujifunza kwa mashine anajikita zaidi katika kusaidia mifumo ya AI kufikia hitimisho sahihi na la haraka zaidi kwa tatizo moja.

Wote wawili wanaweza kutumia maarifa yao katika kila aina ya tasnia na ingawa mara nyingi walianza kusoma sayansi ya kompyuta, wanaweza pia kuwa wabobezi baada ya kusoma hisabati, takwimu, au sayansi zingine zinazohusiana.

2. Mtaalamu wa uendelevu wa mazingira

Inafanya kazi na makampuni ili kufikia malengo yao ya uendelevu wa mazingira.

Ukifanya kazi hii utakuwa mshauri ambaye majukumu yake yanabadilika kulingana na shirika unalofanyia kazi.

Inaweza kujitolea, kwa mfano, kusimamia miradi ya kupunguza uzalishaji wa gesi inayochafua mazingira, kupunguza matumizi ya nishati au kushiriki katika uundaji wa sera za mazingira katika mipango ya uwekezaji.

tt

Chanzo cha picha,asmoh online

Kwa sababu uwanja wako wa kazi ni mpana sana, hakuna "njia moja" ya kuwa mtaalamu wa uendelevu.

Ingawa mtaalamu wa aina hii huwa na masomo yanayohusiana na sayansi ya mazingira, inahitaji ujuzi wa kukusanya na kuchanganua data, kutambua matatizo na kupendekeza masuluhisho ambayo yanafaa kwa kampuni.

3. Mchambuzi wa Ujasusi wa Biashara

Mchambuzi wa ujasusi wa biashara (BI) husoma na kuchambua data ili kusaidia kampuni kufanya maamuzi ya biashara.

Kwa kuchakata kiasi kikubwa cha habari, mchambuzi hutambua hatari zinazoweza kukumba biashara na kupendekeza mabadiliko ili kuboresha ufanisi na tija ya kampuni.

tt

Chanzo cha picha,asmoh online

Kwa ufupi, mtaalamu huyu husoma michakato ndani ya kampuni, hukagua na kuchanganua data ya mshindani, hutambua fursa, na kupendekeza jinsi ya kushughulikia changamoto za biashara.

Mtaalamu huyu pia anachanganya maarifa ya sayansi ya kompyuta, sayansi ya data, takwimu, usimamizi wa biashara, uchumi na nyanja zingine zinazohusiana.

4. Mchambuzi wa usalama wa habari

Makampuni yanakabiliwa na uvujaji wa data nyeti ya biashara au mteja, ikiwa ni pamoja na nambari za kadi ya mkopo, neno la siri au nywila na taarifa za faragha za mamilioni ya watumiaji.

Mchanganuzi wa usalama wa habari amejitolea kulinda mitandao ya kompyuta, mifumo, hifadhidata na aina yoyote ya taarifa nyeti dhidi ya mashambulizi ya mtandaoni.

Kutokana na hili, mtaalamu hufanya kazi ya kurekebisha, kufuatilia, kudhibiti mifumo ya ulinzi na kukabiliana na mashambulizi.

Wale wanaoanza kazi wanahitaji kuwa na angalau shahada katika sayansi ya kompyuta au, kwa mfano, uhandisi wa kompyuta. Kulingana na nchi, kuna vyeti maalum vya usalama wa mtandao.

5. Mhandisi wa FinTech

Sekta ya fintech ni mojawapo ya mifumo ya programu inayokua kwa kasi zaidi duniani.

Mhandisi wa aina hii amebobea katika masuala ya fedha ya kiteknolojia, kama vile huduma ya benki kwa njia inayozingatia akili bandia, usimamizi wa mifumo inayohusiana na kuridhika kwa wateja katika ulimwengu wa kifedha, usindikaji wa malipo ya kidijitali, miamala ya kuvuka mipaka kwa msingi wa cryptography, usimamizi wa mali dijitali, au uchanganuzi wa data kwa ajili ya kudhibiti hatari.

tt

Chanzo cha picha,asmoh online

Anayefanya kazi hii anatakiwa kuwa na ujuzi wa sayansi ya kompyuta na utaalam katika FinTech, akipata maarifa ya akili ya bandia na kujifunza kwa mashine atakuwa amebobea katika nyanja hii ya teknolojia.

Ataweza kushughulikia lugha tofauti za programu, kama vile JavaScript, Python, Ruby, PHP, HTML na CSS. Pia atafanya kazi na hifadhidata kubwa na majukwaa ya cloud.

6. Mchambuzi wa data na mwanasayansi wa data

Usipokuwa makini utafikiaria kazi ya wataalamu hawa wawili inaweza kuonekana kuwa kitu kimoja.

Kwani wote wawili hutafuta mitindo katika data ambayo ni muhimu kwa wateja wao.

Tofauti ni kwamba mwanasayansi huwa na jukumu zaidi na kwa hiyo kwa kawaida iko katika ngazi ya juu kwa cheo.

Mwanasayansi anafanya kazi katika kutunga maswali yake kuhusu data au kuunda miundo kwa kutumia kujifunza kwa mashine, huku mchanganuzi akitsaidia timu ambazo tayari zina malengo.

tt

Chanzo cha picha,asmoh online

Wanasayansi wengi wa data wanaweza kuanza kazi zao kama wachambuzi au wanatakwimu. Hata hivyo wataalamuwote wawili wana uwezo wa kutoa taarifa za maana na kuzitafsiri.

Na wote wawili huendeleza ujuzi katika uwanja wa takwimu na programu ya juu.

Mtaalamu mwingine ambaye ni sehemu ya aina hii ya utaalamu ni mhandisi wa data, ambaye hushughulikia kiasi kikubwa cha data na kuunda miundomsingi ya kidijitali ili kuzibadilisha na kuzihawilisha.

7. Mhandisi wa Roboti

Anasaidia kuunda mifumo ya roboti ambayo hutumiwa kufanya kazi za binadamu na na zile zisizofanywa na binadamu.

Mhandisi huyu huunda mifano ya mifumo ya roboti, huunda, hutunza, na kukarabati mashine, na vile vile hufanya utafiti na kuunda programu mpya za roboti zilizopo.

tt

Chanzo cha picha,asmoh online

8. Mhandisi katika masuala ya electrotechnology

Fani hii imejikita katika kubuni na kuongoza uendeshaji wa mifumo, vipengele, magari na vifaa vya elektroniki, umeme na mawasiliano ya simu.

Inahusiana na usimamizi wa mifumo ya udhibiti kufuatilia utendaji na usalama wa mifumo yote ya umeme na elektroniki katika kampuni.

Ujuzi wake unamruhusu mtu kufanya kazi katika aina tofauti za mifumo ya uzalishaji wa umeme na usambazaji.

Unaweza pia kuweka viwango vya udhibiti ili kufuatilia utendakazi na usalama wa mifumo ya umeme, kielektroniki na mawasiliano ya simu.

Uhandisi wa teknolojia ni neno pana linalojumuisha wataalamu maalumu kama vile wahandisi wa umeme, wahandisi wa kielektroniki, na wahandisi wa mawasiliano ya simu.

Wataalamu hawa hufanya kazi na mafundi katika kila eneo la utaalamu.

9. Mwendeshaji wa zana za kilimo

Kazi yake kubwa ni kuendesha mashine za kusaidia shughuli za kilimo, kama vile kulima, kupanda na kuvuna mazao, kulisha mifugo, kuondoa taka zao.

Unaweza pia kufanya kazi kama vile kuweka maganda, kumwagilia maji, kuendesha magari, au zile zinazohusiana na kushughulikia vifaa vinavyotumika baada ya kuvuna kwa kukoboa, kupura na kurarua.

tt

Chanzo cha picha,asmoh online

10. Mtaalamu wa mabadiliko ya kidijitali

Kadiri mageuzi ya kiteknolojia yanavyoendelea kwa kasi isiyokuwa ya kawaida, mtaalamu wa mabadiliko ya kidijitali ni mtaalamu mkuu katika makampuni kuchukua fursa ya zana zinazopatikana na kuendeleza biashara zao.

Ndiyo maana mtaalamu huyu anahitaji "kuzama" katika kampuni ambayo anafanyia kazi, kuelewa kile anachohitaji na kuendeleza mpango wa mabadiliko ya kidijital.

tt

Chanzo cha picha,asmoh online

Yeye ni sehemu ya timu ya wataalam ambao hufanya kazi kama vile kuanisha teknolojia za kampuni zilizopo, kuongeza mpya, kutoa mafunzo kwa wafanyikazi wa kampuni, kushirikiana katika mpito wa utiririshaji tofauti wa kazi na mifano ya kazi iliyobadilishwa kwa zana mpya za kiteknolojia.

Maoni