SABABU 12 ZA MWANAUME KUSHINDWA KUTUNGISHA MIMBA
Watu wengi wamekuwa wakidhani kuwa mwanamke pekee ndiye mwenye wajibu wa kuhakikisha anapata mimba na ikitokea akakaa muda mrefu kwenye ndoa bila hilo kutokea, basi jamii inamtupia lawama wakiamini tatizo ni lake na siyo mumewe.
kitaalamu ni kwamba tatizo linaweza kuwa kwa mwanaume au mwanamke au wote wawili wana matatizo, tena makubwa.
SABABU 12 NI HIZI HAPA CHINI
1.Korodani kushindwa kushikana vizuri "Undrescended test", hii hutokea baada ya vichocheo (Hormone) kupata hitilafu na kuweza kuleta matatizo ya uzalishaji wa mbegu za kiume ambazo kitaalamu huitwa "Spermatogensis" ingawa vitu kama mrija wa kutolea mbegu unakuwepo lakini huwa hakuna mbegu zinazozalishwa.
2.Tatizo la kimaumbile ambapo kwenye mrija wa kutolea mbegu, pamoja na mkojo, yaani Urethra huota sehemu ya chini ya uume, hivyo kusababisha mbegu kutoweza kufika sehemu ya ndani ya uke, tatizo hili kitaalamu huitwa Hypospadias.
3.Korodani kupata joto sana, kitaalamu huitwa Termal Factor.
Hali hiyo huleta hitilafu kwenye korodani na kusababisha mbegu zisitoke zikiwa na afya nzuri. Tatizo hili huwakumba zaidi madereva wanaosafiri safari ndefu kwa zaidi ya siku mbili.
4.Magonjwa ya zinaa kama yale yanayosababishwa na bakteria aina ya Chlamydia na kusababisha tatizo la uzazi kwa mwanaume au tatizo la tezi za shingoni Mumps ambazo huathiri korodani na kusababisha mbegu kutozalishwa, hivyo kusababisha tatizo la uzazi kwa mwanaume.
5.Kuvuta sigara kwa wingi, kunywa pombe kupita kiasi kwani vitu hivyo husababisha hitilafu ya kuzalisha mbegu.
6.Matatizo ya kurithi ambayo kitaalamu huitwa Chromosomal huweza kusababisha mwanaume asiweze kumpa mimba mwanamke kwani mbegu za kiume huwa chache na hazitoshelezi kusababisha mimba.
7.Kupigwa miale kama ya Ex ray, CT Scan, matumizi ya dawa za vidonda vya tumbo, dawa za presha, dawa za kuzuia degedege pia huathiri utengenezwaji wa mbegu za kiume.
8.Ukosefu wa nguvu za kiume ambao kitaalamu huitwa Erectle Dysfunction au mwanaume kuwa hanithi Impotence kunaweza kusababisha ashindwe kumpa mimba mwanamke.
9.Unene pamoja na mtindo ya maisha. siku hizi watu kuketi vipindi kirefu bila kufanya mazoezi kunachangia. Pamoja na mabadiliko kwenye lishe na kemikali nyingi ambazo zipo kwenye mazingira huongeza kutokuwa na uwezo wa kutungisha mimba.
10.Dawa za kuua wadudu, kemikali zinazoingilia mfumo wa homoni mwilini na mfadhaiko vinatazamwa kama mambo yanayochangia sana katika tatizo hili.
11.Ulaji wa nyama iliyopitishiwa viwandani huongeza mianya ya kushindwa kutungisha mimba.
12.Kuongezeka kwa visa vya saratani ya korodani, visa vingi vya wavulana kuzaliwa bila korodani zote mbili au bila korodani moja, pamoja na kubadilika kwa viwango vya homoni aina ya testosterone husababisha tatizo.
HALI HALISI
Takwim za Wahudumu katika kliniki za masuala ya uzazi wanasema kiwango cha mbegu za uzazi zilizo bora kimekuwa kikishuka kwa takriban asilimia 2 kila mwaka.
Kushuka huku kwa kiwango cha mbegu za kiume kumeshuhudiwa miongoni mwa wanaofika kutaka kutoa mbegu za kutumiwa kuwatungisha mimba wanawake na wale wanaofika wakitaka wasaidiwe kuongeza kiwango cha ubora wa mbegu za uzazi ndipo waweze kutungisha mimba.
Kudhoofika pakubwa
Utafiti umeonyesha kwamba mbegu za kiume zimekuwa zikidhoofika pakubwa kiasi kwamba zinashindwa kuogelea kwenye majimaji ya mwanamke zikielekea kufikia yai kutungisha mimba.
Idadi ya wanaume wanaoomba usaidizi kutungisha mimba imeongezeka mara saba katika mataifa ya mengi katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.
Jali Afya Yako Penda kufanya check up ya Afya yako Zingatia Ulaji bora Fanya mazoezi ili uweze kuwa na Afya Bora.
Maoni