BAWASIRI {HEMORRHOIDS/PILE
Ni ugonjwa unaotokana na kuvimba kwa mishipa ya damu katika mfereji wa njia ya haja kubwa na kuoelekea kuota kinyama sehemu ya haja kubwa
Kuna Aina mbili {2} Za Bawasiri.
1.Bawasiri ya ndani- Bawasiri hii hutokea ndani ya tundu la haja kubwa
2.Bawasiri ya Nje-Bawasiri hii hutokea eneo la nje ya Tundu la haja kubwa
CHANZO CHA BAWASIRI
➖ Tabia ya kuketi sehemu moja kwa muda mrefu mfano; madereva
➖ Tatizo sugu la kuharisha
➖ Ujauzito
➖ Uzito wa mwili kupita kiasi
➖ Kufanya ngono kupitia tundu la haja kubwa (kulawitiwa)
➖ Kupata haja kubwa ngumu
➖ Kua na mgandamizo mkubwa tumboni
➖ Kunywa pombe Kupita kiasi
➖ Kula sana nyama nyekundu
➖ Vidonda vya tumbo
➖ Ngiri(Chango/Hernia
➖ Kula sana pilipili
➖ Kunyanyua vitu vizito
DALILI ZA BAWASIRI
➖ Kupata muwasho mkali katika eneo la juu la haja kubwa
➖ Kujitokeza kwa kinyama eneo la haja kubwa
➖ Kutokewa na kiuvimbe katika tundu ya haja kubwa
➖ Kupata kinyesi chenye damu na maumivu
Maoni