YAFAHAMU MAGONJWA YANAYOATHIRI MFUMO WA MZUNGUKO WA DAMU KIUJUMLA(blood circulation system diseases):
Tunafahamu kuwa mzunguko wa damu unajumuisha ogani kama MOYO na MISHIPA YA DAMU, wakati mwingine mzunguko wa damu huitwa CARDIOVASCULAR SYSTEM.mfumo huu kazi yake kuu ni kusambaza virutubisho na hewa safi ya oksjeni sehemu za ndani ya mwili.
linapokuja suala la kutambua magonjwa ya mzunguko wa damu jambo la kwanza la kutazamwa ni ubora wa utendaji kazi wa moyo na MISHIPA yake ya damu ,kwa maana hiyo hapo ndio utafahamu unashida gani kwenye mzunguko wako wa damu.
HAYA NDIO MAGONJWA 14 HATARI YANAYOATHIRI MZUNGUKO WA DAMU MWILINI:
1.ATHEROSCLEROSIS:
huu ni ugonjwa unaoathiri mishipa ya damu hasa ateri kuwa migumu/ugumu kuliko kawaida,hali hii husababishwa na ulaji wa vyakula vyenye mafuta sana,hali ambayo hufanya mafuta kujirundika ndani ya mishipa hii ya damu na baada ateri kushindwa kulegea na kuwa ngumu kupotisha damu safi.
-ugonjwa huu ndio chanzo kikuu cha ugonjwa mwingine wa SHINIKIZO LA JUU LA DAMU (HYPERTENSION),Ugonjwa huu husababisha matatizo kama FIGO,moyo,na KIHARUSI.
2.SHAMBULIO LA MOYO( HEART ATTACK):
ugonjwa huu kwa jina lingine kitaalamu huitwa MYOCARDIAL INFARCTION (MI), Shambulio la moyo hutokea pale damu inayoingia ndani ya moyo na kutoka kukata ghafla kufika kwenye moyo,halo hii wakati mwingine husababishwa na kuganda kwa damu( blood clot).
3.MAGONJWA YA VALVU ZA MOYO( MITRAL VALVES DISEASES):
valvu za moyo hufanya kazi ya kusukuma ( pump) damu yenye hewa safi ya oksjeni ndani ya moyo na kusambaza sehemu za mwili.magonjwa ya valvu za moyo kufeli hutokea pale valvu hizi za moyo kuvujisha damu na kushindwa kufunga kabisa.hali hii hufanya damu kushindwa kusukumwa kabisa na kurudi ilipotoka kitaalamu magonjwa haya ni kama MITRAL VALVES PROLAPSE,MITRAL VALVE REGURGITATION.
pia ugonjwa wa valvu za moyo uitwao MITRAL STENOSIS ugonjwa huu wa moyo hutokea ambapo valvu za moyo kuwa nyembamba kitu ambacho kinaweza kuizuia damu kutembea haraka .valvu za moyo lazima ziwe imara muda wote ili damu uweze kusukumwa vizuri.
4.ANGINA PECTORIS:
ni miongoni Kati ya magonjwa ya mzunguko wa damu ambao hutokea pale moyo inaposhindwa kupokea damu ya kutosha damu unakuwa chache mno kufika kwenye moyo.hali hii huwapata watu wengi kujihisi maumivu ya kifua ( chest pain),
Watu wenye ugonjwa huu huwa na dalili kama kujihisi kuchoka sana,Kupumua KWA shida, na Kichefuchefu.
5.ARRHYTHIMIA na DYSRHYTHMIA:
magonjwa haya na uhusiano wa pamoja japo hutokea tofauti Katika hali ya Mapigo ya moyo:, Arrhythmia inamaana kuwa hakuna Mapigo yeyote ya moyo na DYSRHYTHMIA inamaana Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida( abnormal heart rate). haya ni miongoni Kati ya magonjwa ya mfumo mzima wa mzunguko wa damu.
6.CARDIAC ISCHEMIA:
ugonjwa huu ni miongoni Kati ya magonjwa ya mzunguko wa damu hasa Katika MOYO , ugonjwa huu hutokea ambapo misuli ya moyo inaahindwa kupata hewa ya oksjeni kabisa ,halo hii hupelekea moyo kushindwa kufanya kazi yake vizuri .watu wenye halo hii hujihisi maumivu kifuni na kuhisi dalili za Shambulio la moyo.
7.HIGH CHOLESTEROL ;
hii ni hali ya mwili kuwa na lehemu isiyo ya kawaida / lehemu mbaya.ni miongoni Kati ya magonjwa yanayoathiri mzunguko wa damu hutokea pale mafuta yapojikusanya sehemu za kuta za mishipa ya damu na kuleta matatizo makubwa ya kiafya Katika mfumo mzima wa damu NB .USIFURAHI KUWA MNENE NI TATIZO
8.HEART FAILURE ( moyo kufeli); ugonjwa huu ndio husumbua watu wengi mno.ugonjwa huu unamaana kuwa moyo inashindwa kabisa kusukuma damu sehemu zote za mwili au KWA uchache mno na huu ugonjwa ndio chanzo cha wahanga kutumia mitungi ya oksjeni hospitalini.watu wenye halo hii hujihisi Kupumua KWA shida,uchovu,kukohoa na wakati mwingine kutaka kutembea tu ili kuleta uchangamfu wa mwili.
9.HIGH BLOOD PRESSURE/HYPERTENSION ( shinikizo la juu la damu);
ugonjwa huu ndio hulalamikiwa na watu wengi wenye umri mkubwa,shinikizo la damu hutokana na msukumo mkubwa wa damu ndani ya mishipa ya damu iliyopita kiasi( abnormal blood pressure).,watu wenye halo hii wanna dalili kama upungufu wa kuona,matatizo ya FIGO,moyo kufeli,Shambulio la moyo na kukosa kabisa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.( Sexual dysfunction).
10.STROKE( KIHARUSI);
KIHARUSI hutokea ambapo moja Kati ya mishipa ya damu kupasuka kunakoweza kusababishwa na mrundikano wa mafuta na kuganda kwa damu,halo hii hufanya hewa safi ya oksjeni kushindwa kufika sehemu za ubongo.
11.PERIPHERAL ARTERY DISEASES (PAD)
ugonjwa huu hutokea mishipa ya ateri inapokuwa miembamba sana Katika sehemu za mwili zifuatazo za mwili kama miguu,tumbo,mikono,na kichwa ;halo hii hupunguza kasi ya damu kutembea na huweza kuharibu SELI za mwili na tisho hasa miguuni;ugonjwa huu ndio unauhusiano mkubwa na ugonjwa wa mfumo wa FAHAMU ( peripheral neuropathy) ,watu wenye hali hujihisi miguu kuwaka moto nyakati tofauti na huwakumba watu wazima sana.
12.VENOUS THROMBOEMBOLISM/THROMBOSIS;
Ugonjwa hutokea Katika halo ambapo damu huganda Katika mishipa ya vena.ugonjwa huu huweza kuzuia mawasiliano Katika mzunguko mzima wa damu mwilini,ni miongoni Kati ya ugonjwa unahitaji uangalizi mkubwa wa kimatibabu.
13. AORTIC ANEURYSM;
Ugonjwa huu huathiri sana sana mishipa mikuu ya ateri ndani ya mwili na kufanya kuta za ateri kuwa dhaifu au Kutanuka na kuvimba.wakati mwingine huweza kupasuka kabisa.
14.ANEMIA
huu ni miongoni Kati ya magonjwa ya mzunguko wa damu mwilini ambao hutokea pale damu inapopungukiwa chembechembe nyekundu za damu ambazo husaidia damu kuwa na hewa ya kutosha ya oksjeni,hivyo mtu mwenye hali ya Kupungukiwa damu mwili wake utashindwa kupokea virutubisho na hewa safi kwenye mzunguko wake wa damu.
Anemia humkumba mtu wa rika lolote.
Tunaendelea nakipindi cha IJUE ELIMU AFYA YAKO
Maoni