MATATIZO YA MFUMO WA MMENG'ENYO WA CHAKULA
VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo ni michubuko au makovu yanayotokea ndani katika Kuta za tumbo au katika Kuta za utumbo mdogo.
Vidonda hivi husababishwa na bacteria anayeitwa *Helicobacter pylori* (H. pylori) ambaye huharibu utando unaokinga Kuta za utumbo kutokuharibiwa na tindikali (acid), hivyo hisababisha ukuta wa Utumbo kuharibiwa na tindikali na kupelekea vidonda katika Kuta hizo za tumbo.
AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO
Kuna aina mbili za vidonda vya tumbo:-
i/Vidonda vya tumbo kubwa: hivi ni vidonda vya tumbo vinavyotokea ndani kwenye tumbo kubwa
ii/Vidonda vya utumbo mdogo: hivi ni vidonda vya tumbo vinavyotokea kwenye utumbo mdogo(hasa juu)
SABABU ZINAZOPELEKEA VIDONDA VYA TUMBO
i/ Bacteria anayeitwa Helicobacter pylori (H. pylori)
ii/ Matumizi ya mda mrefu ya dawa aina ya NSAIDs- Nonsteroidal anti-inflammatory drugs( mfano: ibuprofen, aspirin, Diclofenac)
iii/Tumbokuunguzwa na kemikali
NB: Stress zinaweza sababisha vidonda vya tumbo kwasababu mtu akiwa na stress inapelekea mwili kuzalisha acid nyingi mwili ambayo inaweza kusababisha mtu Kupata vidonda vya tumbo.
Pia kuluka chakula ( skipping meals) inaweza sababisha mtu Kupata vidonda vya tumbo.
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
1:Kiungulia au Maumivu makali kuungua katikati ya kifua
2:Tumbo kujaa Gesi na kuvimbiwa
3:Kutapika damu
4:Kupata Maumivu makali ya tumbo yanayokuwa Kama moto mkali
5:Kupata haja kubwa ya rangi ya kahawia na nyeusi yenye harufu mbaya sana
MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBO
1:Kupata Saratani ya tumbo
2:Kuziba kwa njia ya chakula
3:Kuathiri ini na kongosho
4: Kusababisha tundu katika tumbo na kusababisha tumbo kutoboka kwa ukuta wa tumboni kipindi hiki cha afya kinaishiya hapa tutaendelea siku ya kesho mwenye maswali kalibuni kwa maswali na majibu japo kipindi kitaendelea majaliwa kesho asubuhi
Maoni