SIRI YA MAJIMAJI YANAYOTOKA UKENI IWE BAADA YA TENDO LA NDOA AU WAKATI WA TENDO LA NDOA.
Ivi ulishawahi kujiuliza au kufikiria majimaji yanayotoka ukeni na yenye rangi tofauti tofauti huwa na maana gani na yanaashiria nini iwe ni baada ya tendo au wakati wa tendo la ndoa? Basi nimekuletea ujumbe huu kwa ajili yako soma mpaka mwisho
Kutokwa na majimaji au ute katika via vya uzazi vya mwanamke ni jambo la kawaida wakati ambao mwanamke bado ana umri wa kuzaa, ikiwa ni sehemu ya mwili katika kuondoa sumu au kemikali.
Ute huu kwa kawaida hauna rangi hadi ukikauka juu ya nguo ya ndani ndiyo huashiria rangi nyeupe au njano. Hata hivyo, hali hii huwa kwa kiasi kidogo ambacho hakihitaji mwanamke kuvaa kitu kingine zaidi ya nguo ya ndani ya kawaida ili kuuzuia.
Lakini majimaji hayo huashiria ugonjwa wa hatari yanapokuwa yanaambatana na dalili zifuatazo, naomba uwe makini na uzingatie kabisa:
Maji maji au ute kubadilika rangi na kuwa kama maziwa mtindi, chokleti, njano, kijani, rangi ya usaha, au rangi ya juisi ya parachichi.
Majimaji yakiambatana na harufu mbaya hata kama mwanamke ameoga na kuvaa vizuri. Kuna wakati harufu inakuwa kama shombo la samaki hasa wakati wa kushiriki tendo la ndoa au baada ya tendo la ndoa.
Ute unapozidi kiwango chake cha kawaida cha kila siku (abnormal quantity of discharge).
Maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo
Kuwashwa sehemu za nje na ndani za via vya uzazi vya mwanamke.
Via vya uzazi kuwa na rangi nyekundu kuliko rangi yake ya ngozi ya siku zote.
Muwasho sehemu za mlango wa via vya uzazi kwa ndani.
Maumivu chini ya kiuno, mbele na nyuma, pia chini ya kitovu na hasa kushoto au kulia.
Sehemu ya nje ya via vya uzazi kuwa nyekundu na wakati mwingine wekundu huo kuambatana na michubuko, vidonda na maumivu.
Kama na ww unachangamoto ya kutokwa na maji maji ambayo hauyaelewi toa Comments yako upate elimu zaidi bure pamoja na ushauri nini cha kufanya karibu sana.
Maoni