Njia salama za kupunguza maumivu kipindi cha hedhi.

 Njia salama za kupunguza maumivu kipindi cha hedhi.

πŸ‘‰πŸ» Maumivu kipindi cha hedhi maumivu ya hedhi Maumivu kipindi cha hedhi ni kitu kinachokosesha raha na kukera sana kwa wanawake wengi. 

πŸ‘‰πŸ» Maana kinaweza kutatiza shughuli zako za kila siku kama masomo, biashara na hata shuguli za kiofisi. 

πŸ‘‰πŸ» Tatizo la maumivu kipindi cha hedhi kwa kitaalamu tunaita *dysmennorrhea* .

πŸ‘‰πŸ» Tumeleta kwenu makala hii yenye uchambuzi wa kina kwa tatizo hili linalowatesa kinamama wengi na wadada. 

πŸ‘‰πŸ» Utajifunza nini maana yake, tatizo linaanza vipi na namna gani utumie njia rahisi nyumbani kwako kupunguza makali ya maumivu. *Dysmenorrhea Ni Kitu Gani?* 

πŸ‘‰πŸ»πŸ˜ŒDysmenorrhea ni

πŸ‘‰πŸ»jina la kitabibu kwa maumivu kipindi cha hedhi.

πŸ‘‰πŸ» Maumivu ambayo hutokana na kusinyaa kwa misuli ya mji wa mimba. 

πŸ‘‰πŸ» Wakati wa hedhi misuli husinyaa, ili kuruhusu kumeguka kwa ukuta na kutoa damu iliyochanganyika na yai ambalo halikurutubishwa nje. 

πŸ‘‰πŸ» Maumivu haya yamegawanyika katika aina mbili

Soma nakala inayo fata hapo chiniπŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ» *Aina Ya Kwanza Ya maumivu ya Kawaida*

πŸ‘‰πŸ» (Primary Dysmenorrhea)

Maumivu haya ni ya kawaida kabisa kwa wanawake wanapopitia kipindi hikia ambacho hujirudia kila mwezi.

πŸ‘‰πŸ» Maumivu kikawaida huanza kati ya siku moja ama mbili kabla ya hedhi kuanza kutoka.

πŸ‘‰πŸ» Mwanamke hujiskia mamumivu haya kwenye tumbo la chini, kwenye nyonga na kiuno kwa ujumla.

Maumivu haya yanaweza kuwa madogo au yakawa makali sana na huisha ndani ya masaa 12 mpaka 72. Yanaweza kuambatana na kutapika na kupata kizunguzungu. Kwa wanawake wengi maumivu haya ambayo ni ya kawaida kabisa hupungua kadiri umri unavoenda na pia pale mwanamke akijifungua. 


Maumivu Aina Ya Pili Yasiyo Ya Kawaida (Secondary Dysmenorrhea) 

πŸ‘‰πŸ» Maumivu haya ni kutokana na tatizo fulani la kiafya kweye via vya uzazi vya mwanamke.

πŸ‘‰πŸ» Changamoto kama vile uvimbe ambayo siyo wa saratani ndani ya mfuko wa mimba (uterine fibroids), kukua kwa tishu laini za mfuko wa mimba kuelekea kwenye viungo vingine kama uke na mifuko ya mayai (endometriosis).

πŸ‘‰πŸ» Na pia kupanuka kwa ukuta wa uterus kutokana na kukua kwa tishu za ndani za uterus kuelekea ukuta wa nje (adenomyosis).

 πŸ‘‰πŸ» Maumivu haya pia yasiyo ya kawaida yanaweza kuwa yamesababishwa kwa athari za bacteria ama virusi katika via vya uzazi.

πŸ‘‰πŸ» Kikawaida maumivu haya huanza mapema zaidi wakati wa hedhi ya huchukua muda mrefu zaidi kuisha ukilinganisha na maumivu yake ya kawaida (primary dysmenorrhea). 

πŸ‘‰πŸ» Na pia maumivu haya yanakuwa hayaambatani na kutapika, kuharisha, kizunguzungu wala kukosa nguvu na ganzi. Nini Chanzo Cha Maumivu Kipindi Cha Hedhi?

πŸ‘‰πŸ» Maumivu haya hutokana na kitendo cha misuli ya uteras kukaza na kusinyaa. 

πŸ‘‰πŸ» Kitendo hichi huratibiwa na homoni ya prostaglandins. 

πŸ‘‰πŸ» Ni kawaida kwa uterus ambao ni mfuko unaobeba mimba kusinyaa kipindi chote cha mzunguko wa hedhi ambacho huchukua siku 28.

πŸ‘‰πŸ» Lakini utofauti ni kwamba wakati wa kutoa hedhi yenyewe mfuko huu husinyaa na kujikaza zaidi na hivo kukatisha hewa safi ya oyygen kufika kwenye misuli ya mfuko huu wa mimba.

πŸ‘‰πŸ» Maumivu ni matokeo ya kukosekana kwa muda kwa hewa ya oxygen kwenye baadhi ya misuli ya uterus.

Ni Kipindi Gani Unatakiwa Kumuona Daktari Ili Kupata Matibabu Na Ushauri Zaidi.

Kama maumivu yako ni makali zaidi kuliko kawaida na yanachukua zaidi ya siku . Hakikisha unamwona daktari wako haraka, kwanini?. Kwasababu yawezekana maumivu yako siyo ya kawaida na yaweza kuwa una uvimbe ama maambukizi ya bacteria na virusi kwenye mfuko wa mimba.

Hivo kuwahi hospitali itasaidia kutibu tatizo lako mapema kabla halijawa kubwa. Pia tunashauri kuwahi kumwona dactari kwa sababu ukuaji wa tishu za mfuko wa mimba unahusishwa na kusababisha saratani ya shingo ya kizazi, na hivo kujua chanzo cha tatizo lako mapema kutasaidia kulitibu mapema.

Maoni