NDOA YAKO ITAISHIA KWENYE TALAKA, ENDAPO ZIPO DALILI HIZI

NDOA YAKO ITAISHIA KWENYE TALAKA, ENDAPO ZIPO DALILI HIZI MAFUNZO YA ELIMU YA'AFYA YAPO  LAKINI TAMBUA.

Ili mahusiano yetu yadumu basi katika nyanja hii ya ukosoaji inatubidi tuwe makini sana. Ni lazima tujifunze kuwa watu wa kulalamika juu ya makosa ya wapenzi wetu kuliko kuwa watu wa kukosoa. 

Ukihitaji kuepuka kuwa mkosoaji basi jifunze kujua katika hilo baya/kosa lililotendwa na mwenzi wako wewe urmeumia juu ya nini na unataka kipi kitendeke ili mambo yaende sawa.


Gottman anasema kwamba inakupasa ujifunze kuepuka kuuongelea vibaya utu (personality) wa mwenzi wako. Acha kuchokonoa tabia zake Kwa lugha ya moja kwa moja. Epuka kutumia maneno kama "ona ulivyo msahaulifu, kwanini hujielewi, sijui ukoje, unakera sana, hupendi kuwa muelewa, upo upo tu" 


Ifuatayo ni mifano ya kuweza kutofautisha kati ya Ulalamikaji (complaint) na ukosoaji (criticism).


•Kulalamika: Hakuna gesi kwenye jiko, kwanini hukuweka na fedha nilikuachia na wewe mwenyewe ulisema utaweka.

•Kukosoa: Kwanini huwa hukumbuki vitu wewe, hivi nimekwambia mara ngapi juu ya kujaza gesi na ukasema utafanya. 


•Kulalamika: Ilibidi unipe taarifa kuhusu kuja kwa marafiki zako, ki ukweli sijapendezwa na tabia hii.

•Kukosoa; Kwanini unawapa kipaumbele sana marafiki zako, mbona hukukumbuka kunipa taarifa kama watakuja. Sijapenda kabisa. 


Hata hivyo Gary Chapman, mwandishi wa kitabu cha 'The five love of language'  katika mbinu yake namba Moja ya 'Words of affirmation' aliwahi kusema asilimia 99 ya mahusiano yetu na interactions zetu dhidi ya watu mbali mbali yamejengwa katika msingi wa maongezi. Ni jinsi gani unatumia kinywa chako, ni jinsi gani maongezi yako yanagusa moyo wa mtu anaekusikiliza. Hivyo katika hili sisi kama wapenzi ni lazima tulizingatie kwenye mahusiano yetu. Zalau haitakiwi  kwa ninyi ambao mupo katika mahusiano mkubwa

  HEKIMA IKUONGOZE KUCHUNGUZA HAYO ITAKULINDA NA ULIMWENGU

Maoni