MIMBA KUTUNGISHWA NJE YA MJI WAMIMBA(UTERUS) (ECTOPIC PREGNANCY)

MIMBA KUTUNGISHWA NJE YA MJI WAMIMBA(UTERUS)
(ECTOPIC PREGNANCY)

Katika kielelezo chetu hapo juu, mimba ilitakiwa ikae eneo A``` 

Chanzo, Dalili, na matokeo.

Kila mmoja anatamani kuwa na familia yenye watoto anaowahitaji. Lakini kwa bahati mbaya si watu wote wamefanikiwa kutimiza ndoto hii kutokana na matatizo mbalimbali hasa yale yahusuyo uzazi.

Kutokana na sababu mbali mbali baadhi ya wanawake wameshindwa kushika mimba au hushika mimba lakini hutoka kabla ya muda wa kuzaa na wengine mimba zao kutunga nje ya mji wa mimba (Uterus) kitaalamu huitwa ectopic pregnancy.

ECTOPIC PREGNANCY ni hali inayotokea kwa mwanamke ambapo yai lililorutubishwa na mbegu ya mwanaume hujitungisha au hujishikiza nje ya mji wa mimba (Uterus).
Kwa kawaida mimba hutungishwa au kushikizwa sehemu moja tu ya kizazi cha mwanamke ambayo huitwa mji wa mimba (Uterus) katika picha yetu Ni eneo lenyewe herufi A, hapo ndipo huishi na kukuwa kitoto mpaka kufikia hatua ya Mama kujifungua.

Kwa baadhi ya wanawake hutokea mimba kushikizwa au kutungishwa sehemu zingine za kizazi , mfano kwenye shingo ya kizazi (cervix) , mji wa mayai (ovary) au kwenye mirija ya uzazi (follopian tubes). Ikitokea hivi, basi hiyo mimba haitaweza kuishi na kukua, kwani hizi si sehemu maalumu kwa ajili ya mimba.

ZIFUATAZO NDIO SABABU ZA MIMBA KUTUNGISHWA NJE YA MJI WA MIMBA

1. Maambukizi (infections) au kuvimba katika kuta za kizazi hasa kuta za mirija ya kizazi kitaalamu huitwa pelvic inflammatory diseases (P.I.D).
2. Upasuaji unaohusisha kizazi au sehemu zinazozunguka uzazi.
3. Kuzaliwa na kizazi ambacho kina umbo la tofauti na kizazi cha kawaida, mfano kuzaliwa na mirija ya uzazi iliyopinda (haijanyooka).

 Je, watu gani wako kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo hili ?

👉Mwanamke mwenye umri zaidi ya miaka 35.
👉Mwanamke ambaye alishawahi kupata tatizo hili yuko kwenye hatari ya kupata tena.
👉 Mwanamke ambaye amewahi kufanyiwa upasuaji unaohusisha kizazi au sehemu zinazonguka kizazi.
👉Mwanamke aliyewahi kuugua P.I.D
👉Mwanamke aliyewahi kutoa mimba.
👉Mwanamke anayevuta sigara.

Je, dalili za kutungisha mimba nje ya kizazi ni zipi?

Dalili za mimba kutungishwa nje ya mji wa] mimba ni :-
🤏Kutokwa na damu ukeni na maumivu ya tumbo.
🤏Maumivu ya tumbo huwa ya kukata, kuvuta au kunyonga nyonga

🤏Kama damu itatoka nyingi hupelekea mapigo ya moyo kwenda kasi, kizungu zungu, kuzimia na maumivu ya kichwa. Lakini pia mwanamke anaweza kupoteza maisha.

 Je, itakuwaje mtu akipata tatizo hili?
🤏Mimba iliyo tungishwa nje ya mji wa mimba haiwezi kukua, hivyo ni lazima itolewe. 🤏Upasuaji maalumu (laparatomy) hufanyika ili kuweza kuondoa mimba iliyotungishwa nje ya kizazi.

Mwisho;
 
 Jifunze kutumia chakula Kama dawa sasa, Ili usitumie dawa Kama chakula baadaye, epuka kifo kisicho cha lazima, Linda Afya yako

Maoni