JE' UNAFAHAMU NINI KUHUSU " STROKE" , " KIHARUSI" AU KUPOOZA

 JE' UNAFAHAMU NINI KUHUSU " STROKE" , " KIHARUSI" AU  KUPOOZA


"TIBA NA KINGA YA KIHARUSI (KUPOOZA) AU STROKE (FAHAMU KIUNDANI)"

Ni ukweli usiojificha kwamba wagonjwa wengi siku hizi wamekuwa wakikumbwa na tatizo hili la kupooza ambalo wengi huwakumba ghafla wakiwa hawana ufahamu wowote nini ambacho kimetokea.

Kabla zijakuelimisha mengi mpendwa msomaji wangu wa Makala zangu, basi leo nakupa maana ya baadhi ya maneno haya:

KUPOOZA

Hii ni ile hali ya kiungo kupoteza utendaji kazi wake kwa sababu ya neva za fahamu kuathiriwa.


KIHARUSI AU STROKE

 Stroke Ni Nini?         Stroke au kiharusi ni tatizo linalotokea ghafla kwenye ubongo ambapo mtiririko wa damu kwenye eneo fulani la ubongo husitishwa ghafla au kupungua sana hivyo kusababisha eneo hilo la ubongo kukosa damu na virutubisho muhimu na seli za eneo hilo kuanza kufa. Hili linaweza kutokea pale mishipa ya damu ya kuelekea kwenye eneo hilo ikiziba au mishipa ndani ya ubongo katika eneo hilo kupasuka. Seli za ubongo za eneo hilo zikianza kufa kwa kukosa damu, shughuli zote zinazoendeshwa na eneo hilo la ubongo husimama kwa mfano kumbukumbu au misuli. 

Kiharusi ni ugonjwa wa dharura hivyo tiba inatakiwa ipatikane mapema iwezekanavyo. Kimsingi kiharusi huweza kumpata mtu ye yote wakati wo wote.

Kuna aina tatu za stroke; ischemic, hemorrhagic na TIA. Kundi la watu lililo kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu ni lile la watu wenye miili mikubwa, umri zaidi ya miaka 55, wenye historia ya ugonjwa huu kwenye familia zao, ambao hawafanyi mazoezi , wanaokunywa sana pombe au kutumia madawa haramu.


Kiharusi Husababishwa Na Nini?

Kila moja ya aina za stroke hapo juu inasababishwa na vitu tofauti.

Ischemic strokes, ndiyo aina ya stroke inayowaathiri watu wengi zaidi, asilimia 85 ya wagonjwa wa stroke hupatwa na aina hii ya stroke. Aina hii ya stroke husababishwa na kuziba kwa arteri (mishipa ya kusafirisha damu safi) zinazoelekea kwenye ubongo au kusinyaa kwa mishipa hiyo hivyo kusababisha hali inayoitwa ischemia (upungufu mkubwa wa mtiririko wa damu).

Kuziba kwa mishipa ya damu hutokea baada ya damu kuganda ndani ya arteri zinazoeleka kwenye ubongo au katika maeneo ya mbali zaidi na kusukumwa kwenye mishipa yenye kipenyo kidogo ndani ya ubongo. Mishipa hii inaweza kuzibwa pia na mafuta yaliyoganda ndani ya arteri (plaque).

Hemorrhagic strokes , husababishwa na arteri ndani ya ubongo kuvuja damu au kupasuka. Damu hii iliyovuja huleta mgandamizo kwenye seli za ubongo na kuziharibu. Kupasuka kwa mishipa ya damu husababishwa na hypertension, trauma au dawa zinazofanya mishipa hii ya damu kupungua unene wake.

Transient ischemic attack (TIA) , hii ni tofauti na aina hizo mbili za stroke hapo juu kwani hapa mtiririko wa damu kuelekea kwenye ubongo huvurugwa kwa muda mfupi kwa sababu zile zile tulizozitaja hapo juu tulipozungumzia ischemic strokes. Stroke ya aina hii ni ishara ya kutokea strokes nyingine baadaye kama hatua zinazostahili hazitachukuliwa

.

 Dalili Za Kiharusi (Stroke)

Ugonjwa wa stroke humpata mtu ghafla na dalili hutokea kwa muda mfupi sana. Dalili kuu za ugonjwa huu ni:

* Kuchanganyikiwa, mtu akipata shida ya kuongea na kuelewa anachoambiwa.

* Maumivu ya kichwa yanakwenda pamoja na kupoteza fahamu kwa vipindi na kutapika.

* Ganzi katika viungo vya uso, mkono na mguu na hasa vikiwa vya upande mmoja wa mwili

* Kupata shida ya kuona kwa jicho moja au yote.

* Kupata shida ya kutembea vikichanganyika na kizunguzungu na kukosa mpangilio wa matendo ya mwili.

* Athari za kiharusi zinaweza kuwa ni za muda mrefu. Kulingana na muda uliopita kabla ya kuugundua na kuutibu ugonjwa huu, mtu anaweza kupata ulemavu wa muda mfupi au wa kudumu. 

* Pamoja na madhara ya stroke kama yalivyo orodheshwa hapo juu, mgonjwa wa stroke anaweza pia kupata yafuatayo:

* Msongo wa mawazo.

* Maumivu kwenye mikono na miguu yanayoongozeka baada ya viungo hivyo kufanya kazi au kutokea mabadiliko ya hali ya hewa.Kupooza au udhaifu wa upande mmoja wa mwili.

* Kupata shida katika kufanya matendo ya kuonyesha hisia za mwili

*Kushindwa kumudu matumizi ya kibofu cha mkojo au viungo vya njia ya haja kubwa.


Dalili zingine za kiharusi au stroke ni:

*Kupoteza fahamu kwa ghafla kwa kipindi fulani cha muda.

* Kupooza ama kupata Udhaifu wa mwili upande mmoja , ama

* Wakati mwingine Pande zote za mwili hupooza.

* Kupoteza uwezo wa kuona kwa ghafla kwa kipindi fulani.

* Kupoteza uwezo wa kuongea ama kushindwa kuumba maneno vizuri

* Kupata ganzi na kuhisi vitu vinakuchomachoma mikononi na miguuni

* Kuchanganyikiwa ghafla(confusion) kwa muda.

* Kukosa balance ya kutembea ama kushindwa kabisa kutembea.

* Kichwa kuuma sana unahisi kama kinapasuka ikiambatana na kutapika(hili huwa halitokei sana kwa wengi).


SABABU ZISIZO EPUKIKA.

1. UMRI

Tafiti zinaonesha kuwa kadri umri wako unavyozidi kuwa mkubwa ndivyo unavyozidi kuwa hatarini sana kukumbwa na tatizo la kupooza. Umri Zaidi ya miaka 50 upo katika hatari kubwa sana ya kupata magonjwa yatakayo kupelekea kupata kiharusi. Kwani kiharusi ni ugonjwa mmoja wapo utakao kupelekea kupooza kwa baadhi ya viungo vya mwili wako na hatimaye mwili mzima.

Hivyo kama wewe bado hujafikia katika umri huu, basi ni wakati wa kuishi katika lishe asili inayotokana katika mashamba yetu ya wakulima.


2. JINSIA

Tafiti zinaonesha kwamba wanaume wako hatarini sana kupata kiharusi ukilinganisha na jinsia ya kike. Lakini pia tafiti zinaonesha kuwa kati ya mwanamke na mwanaume, mwanamke ndiye yupo hatarini sana kupata kifo kitokanacho na kiharusi. Hivyo endapo mwanamke akipatwa na kiharusi maendeleo yake kuanzia anapopatwa na tatizo huwa sio mazuri sana ukilinganisha na mwanaume. Hivyo mwanamke huwahi kukutwa na kifo Zaidi ukilinganisha na mwanaume anaweza kukaa muda mrefu sana.


3. URITHI

Kuna watu wenye historia kuwa katika ukoo wao kuna watu wenye matatizo ya kiharusi au babu, bibi alikumbwa na tatizo hilo. Hivyo hata wewe unaweza ukawa hatarini kupata tatizo kama hilo endapo tu maisha unayo ishi nayo yakiwa ni maisha yasiyo jumuisha lishe ya asili au ninayopenda kuita "lishe ya dawa".


4. KAMA UMESHAWAHI KUPATWA KIHARUSI

Hii ni aina ya kiharusi inayotokea kwa muda mfupi na kupotea. Muda mwingine huwa ni vigumu kutofautisha na kiharusi chenyewe. Maana kiharusi kidogo (Transient Ischemic Attach) husababisha pia viungo kupoteza utendaji kazi wake na inaweza pia kuathiri utendaji kazi wa ubongo kiakili pia. Hivyo kama uliwahi patwa na TIA kipindi cha nyuma, uwezekano wa kupata tena ni mkubwa sana, na unaweza kupata kiharusi kabisa chenyewe.

Hapo juu nimesema kuwa ni vihatarishi visivyozuilika LAKINI ni kwa wale wasioweza kubadili mienendo ya maisha ya kifahari na kujiepusha na magonjwa tabia kama kisukari,shinikizo la damu na kiwango kikubwa cha lehemu ( Cholesterol ) mwilini mwako.


 SABABU ZILIZO NDANI UA UWEZO WAKO.

"YAANI UNAZOWEZA KUZIDHIBITI ILI KUJIEPUSHA NA KIHARUSI ( STROKE)".


1. MAGONJWA YA MOYO

Magonjwa ya moyo kwa umri Zaidi ya miaka 60 imekuwa ni kawaida kutokana na miili yetu kuwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini mwetu na miili yetu kuwepo katika mazingira ya kupokea vyakula visivyo vya msingi katika kuboresha utendaji kazi wa mwili wako na tofauti na kuharibu uwezo wa mwili wako kufanya kazi ipasavyo.


2. KIWANGO KINGI CHA CHOLESTERO(LEHEMU) MBAYA MWILINI MWAKO

Lehemu kwa tafsiri nyepesi ni fati(mafuta) ambayo ipo kama nta ( wax) huzunguka sehmu mbalimbali katika mwili wako kwa kupitia mfumo wa mzunguko wa damu.

Ikumbukwe Lehemu ina kazi kubwa sana miilini mwetu kama kutengeneza seli za mwili na kutengeneza homoni za miili yetu na kazi zingine nyingi. Hivyo basi ningependa kukuambia kuwa kuna aina kuu tatu za lehemu ambazo ningependa kuzitaja kwa ufupi katika makundi makuu mawili, Lehemu mbaya ambayo inajulikana kama Low density Lipoprotein (LDL) pia na Triglycerides na aina ya pili ni lehemu nzuri ijuilikanayo kama Hingh density Lipoprotein –HDL.

Lehemu inaweza kusababisha kiharusi kwa sababu ya tabia yake ya kunasa kiurahisi kwenye kuta za mishipa ya ateri na hatimaye kupunguza kipenyo cha mshipa wa damu au kuziba kabisa na hatimaye kuzuia damu kufika vizuri katika ubongo na hatimaye ubongo hukosa damu na oxygen.

Lehemu hujulikana kama kisababishi kikubwa cha aina moja wapo ya kiharusi kinachosababishwa na mishipa midogo ya damu kutopitisha damu na kuulisha ubongo wako vizuri na hatimaye seli za ubongo huanza kufa nah ii hutokea baada tu ya ubongo kukosa damu kwa muda wa dakika tatu.

Aina hii ya kiharusi huitwa ISCHEMIC STROKE (Ischemia, Ni ile hali cha seli za mwili kufa Kwa kukosa oxygen, na Stroke ni kupooza). Hivyo Ischemic stroke ni kupooza kunako sababishwa na kukosa hewa ya oksijeni kwenye ubongo kwa sababu ya kukosa damu kwenye ubongo kunakosababishwa na kuziba kwa mishipa midogo midogo inayopeleka damu kwenye ubongo .

Pia inashauri kuwa kiwango cha lehemu nzuri yani HDL iwe 50 mg/dl au Zaidi kwa wanawake na kwa wanaume HDL iwe 40 mg/dl au Zaidi.


3. SHINIKIZOLA JUU LA DAMU( HIGH BLOOD PRESSURE)

Shinikizo la damu ni msukumo wa damu ndani ya mishipa ya damu thidi ya ukuta wa mishipa. Shinikizo la damu lenye takwimu ya Zaidi 140/90 mmhg kwa muda mrefu utakuwa unastahili kuitwa mgonjwa wa shinikizo la juu la damu.

Shinikizo kubwa la damu husababisha kiharusi kwa kusababisha mishipa midogo ya damu ya ubongo kupasuka na hatimaye damu kuvia kwenye ubongo. Aina hii ya kiharusi huitwa Hemorrhegic Stroke. Aina hii ya kiharusi ni mara chache sana kutokea na huwa ni nadra sana kukuta mtu ana aina hii ya kiharusi lakini ndio aina nambari moja inayoweza kusababisha kifo haraka sana kwa mgonjwa. Kwani wagonjwa wengi wanaopata aina hii ya kiharusi huwa maendeleo yao sio mazuri na wengi hufika hospitali wakiwa hawajitambui kabisa.

Ugonjwa wa Shinikizo la damu unazuilika kabisa kwa kufuata masharti machache kama haya hapa chini:

Ulaji wa vyakula vya madini ya potasiamu hadi kufikia 3900mg kwa siku kutoka kwenye ndizi,machungwa,matunda yaliyo kaushwa,viazi vitamu nk

Ulaji wa Madini ya Calcium angalau 1200mg kila siku kutoka kwenye vyakula kama mtindi na maziwa ya kuwaida

Ulaji wa vyakula vyenye magnesium angalau 420mg kwa siku kwa wanaume na 320mg kwa wanawake kutoka kwenye vyakula kama Spinachi, mboga za kijani, Ndizi nk


4. KUTOFANYA MAZOEZI YA VIUNGO

Mazoezi siku hizi yamekuwa yakitumiwa na watu pekee wanao hitaji kupunguza mwili na kupunguza nyama uzembe ( belly fats) ,inapendeza sana wadada wengi kuchukia kubadirika kwa miili yao unaotokana na ulaji wa vyakula visivyo asili, Napenda kukuambia kuwa Mazoezi pekee sio


SULUHISHO LA KUPUNGUZA MWILI WAKO, NA WALA SIO SULUHISHO LA KUONDOA NYAMA UZEMBE.

Mazoezi huimarisha viungo na mzunguko wa damu na kusaidia mwili wako kutoa taka ambazo zimepatikana kutokana na shughuli za mwili.

Tafiti zinaonesha kwamba watu ambao hawafanyi mazoezi ya kutosha katika umri mkubwa huwa hatarini kupata kiharusi aina ya Ishemic stroke inayosababishwa na damu kutosukumwa ipasavyo katika mishipa ya damu na kusababisha emboli kunasa kwenye mishipa ya damu na kuzuia damu kufika vizuri katika ubongo.


MAKUNDI MENGINE YALIYO KWENYE HATARI YA KUPATA KIHARUSI

5. Walevi wa pombe na sigara

6. Wanaotumia njia za uzazi wa mpango kwa muda mrefu

7. Watu wenye kisukari kwani kisukari na shinikizo la damu ni bwana harusi na bibi harusi mara nyingi hutembea kwa umoja.


TUNAZO DAWA NZULI ZA KUREKEBISHA TATIZO LAKO NA KUPONA JUMRA 

Maoni