HÀTARI MAISHANI MWAKO UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO - PEPTIC ULCERS

 HÀTARI MAISHANI MWAKO UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO - PEPTIC ULCERS 


 Vidonda Vya Tumbo ni nini?

• Vidonda vya tumbo (Peptic Ulcers) ni ugonjwa unaompata mtu ambapo kunatokea vijitundu au michubuko katika kuta za ndani za viungo vya mfumo wa uyeyushaji chakula.

•  Michubuko hiyo huweza kutokea katika eneo la mfuko wa tumbo, katika duodenum au katika eneo la koo. Inakadiriwa kuwa asilimia 5 hadi 10 ya watu hupatwa na ugonjwa huu angalau mara moja katika maisha yao.

• Huu ni ugonjwa ambao unaweza kumrudia mtu baada ya kupona endapo chanzo chake hakikudhibitiwa. 

• Kama ugonjwa huu utamrudia mgonjwa , mtu huyu atakuwa amejiweka kwenye hatari kubwa ya kupata madhara makubwa zaidi kama kutokwa na damu au kutokea tundu kubwa katika kuta za mfuko wa tumbo.


Dalili za Ugonjwa huu.

• Kukosa hamu na Uwezo Wa Tendo la Ndoa.

• Kuchoka choka sana bila sababu maalum.

• Kuuma mgongo au kiuno..

• Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia

• Kizunguzungu.

• Kukosa usingizi.

• Usingizi wa mara kwa mara.

• Maumivu makali sehemu ya mwili.

• Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali. • Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali

• Kichefuchefu.

• Kiungulia.

• Tumbo kujaa gesi.

•Tumbo kuwaka moto.

• Maumivu makali sehemu kilipo kidonda.

• Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi

• Kutapika nyongo.

• Kutapika damu au kuharisha.

• Sehemu za mwili kupata ganzi.

• Kukosa hamu ya kula.

• Kula kupita kiasi.

•Kusahahu sahau na Hasira bila sababu.


Chanzo Cha Vidonda vya tumbo ?

• Linapokuja suala la nini husababisha vidonda vya tumbo unaweza ukapata stori nyingi bila idadi, lakini kwa kifupi kabisa; vidonda vya tumbo ni ishara za mwili kupungukiwa maji na kama matokeo ya asidi kuzidi mwilini kuliko alkaline. Vinaweza pia kuletwa na bakteria ajulikanaye kama H.Pyroli.


Vitu vifuatavyo vinahusika katika kuleta vidonda vya tumbo mwilini.

👉Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuondoa maumivu.

👉Uvutaji wa sigara.

👉Unywaji wa pombe.

👉Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha.


Madhara ya Vidonda vya tumbo.

Uvujaji wa damu ndani ya utumbo: 

• Hali hii yaweza kusababishwa na vidonda kuenea hadi kwenye mishipa ya damu na hivyo kufanya damu kuanza kuvuja. 

• Hali hii ni hatari sana na inahitaji tiba ya dharura.

• Vidonda vya tumbo huweza kusababisha tundu (kutoboka kwa ukuta wa tumbo) na kufanya vitu vilivyo ndani ya utumbo kutapakaa katika tumbo (abdomen) Hali hii huitwa peritonitis na ni hatari sana na inahitaji matibabu ya dharura. 

• Aidha, kuenea huko kunaweza pia kuathiri tezi kongosho na kusababisha madhara katika tezi hiyo, ugonjwa unaojulikana kama pancreatitis.

• Vidonda vya tumbo vinaweza pia kuenea na kuathiri pia viungo vya jirani kama vile ini au kongosho (pancrease).

• Kuvimba kwa kuta za tumbo pamoja na makovu yanayosababishwa na vidonda hivi huweza kusababisha kuziba kwa njia ya kupitishia chakula kutoka kwenye tumbo (stomach) kwenda sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenum) hali ambayo kitaalamu huitwa gastric outlet obstruction.

• Iwapo vidonda vya tumbo vimesababishwa na H. pylori, kuna uwezekano wa kati ya mara tatu hadi ya sita ya mgonjwa kupata kansa ya tumbo (stomach cancer).


Vidonda Vya Tumbo Vinatibika na Kupona Kabisa


Kwa tiba na ushauri WA MATIBABU MUONE DAKTALI  MOJA KWAMOJA UPATE MATIBABU

Maoni