FAHAMU KUHUSU UGONJWA HATARI WA KIHARUSI(STROKE)


Kiharusi ni ugonjwa wa dharura na hatari ambao hutokea pale seli za ubongo zinapokufa kwa kukosa hewa ya oksijeni na chakula kutokana na kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo.


Aina za kiharusi

Kuna aina kuu mbili za Kiharusi,

1. Kiharusi kinachotokana na kuziba kwa mishipa ya damu ya damu ya ubongo

2. Kiharusi kinachotokana na kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo.


Ukubwa wa tatizo la kiharusi

Kiharusi ni muuaji namba 2: Kwa mwaka 2015 kulingana na ripoti maalumu ya Shirika la Afya duniani WHO kuhusu sababu za vifo ilionesha kiharusi kinashika nafasi ya pili kati ya magonjwa yote kwa kusababisha vifo vingi


Kiharusi husababisha ulemavu kwa wengi: 

Kiharusi kinashika nafasi ya tatu kati ya visabibishi vya ulemavu duniani. Waathirika wengi huishia kuwa walemavu


Dalili za kiharusi

1.GANZI

Mtu anayepata kiharusi hupata ganzi inayoanza ghafla na mara nyingi huathiri upande mmoja wa mwili. Mfano: Upande mmoja wa uso kufa ganzi na kushindwa kuongea vizuri au kutabasamu


2.KUPATA SHIDA KUONGEA

Mgonjwa wa kiharusi hushindwa kuongea vizuri, utoaji wa maneno huwa sio wa kawaida

Mfano: Mgonjwa kushindwa kumaliza sentensi au kuongea kama amelewa sana

-Pia hali hii huweza kuambatana na kutoka mate(udenda) kwa wingi mdomoni


3.KUSHINDWA KUONA

Mgonjwa wa kiharusi anaweza kushindwa kuona, hali hii hutokea ghafla. Inaweza kuhusisha jicho moja au macho yote mawili.

4.Pia mgonjwa anaweza kupoteza fahamu au kupata degedege

5. Mgonjwa anaweza kushindwa kuzuia haja kubwa au ndogo au vyote viwili


VITU VINAVYOCHANGIA MTU KUPATA KIHARUSI

1. Ugonjwa wa Shinikizo kubwa la damu (presha)

2. Uvutaji sigara

3. Ugonjwa wa kisukari

4. Magonjwa ya moyo hasa ugonjwa wa mtetemo wa moyo (atrial fibrillation)

5. Tatizo la mafuta mengi kwenye damu (Lehemu au cholesterol)

6. Uzito uliopitiliza

7. Unywaji wa pombe uliokithiri

8. Kutokufanya mazoezi

9.Tabia ya kukaa kwa muda mrefu sehemu moja

10.Matumizi ya vyakula vilivyosindikwa (fast/junk food)

Ukiamua kuzingatia hayo yote kwa kuepuka visababishi utakuwa umejisaidia zaidi kwani tatizo ili husababishwa na mtu mwenyewe kutokana na mfumo wake wa maisha.

Kama unahitaji ushauri zaidi tunaweza kuwasiliana ili usaidiwe tatizo lako moja kwamoja

Maoni