DHIBITI NGUVU INAYOKUPELESHA NA KUKUFANYA KUPOTEZA TUMAINI LAKO
Nje ya mihemko inayochochea mwili,Kuna Saikolojia inayojifanya mtu awe mtulivu katika kufanya jambo,pale Saikolojia inapofeli kufanya kazi hakika hekima na ufahamu pia hutoweka Kwa mtu Huyo,
ulishawahi sikia mtu anasema yule jamaa Hana hekima kabisa yaani anatukana tusi kama Lile mbele za wazee,au anaongea jambo kama Lile sehemu kama zile maana yake mihemko inampelekesha
-ulishawahi sikia yule jamaa Hana akili kabisa mke wake anamuomba Yeye hamuachii Hela ya matumizi maana yake mke wake apate wapi Hela za matumizi kesho atalalamika mbona mwanamke Malaya kumbe Yeye ndiye hajui namna ya kuishi na mke,hata kama wamegombana ilimpasa Hela ya matumizi kutoa kama kawaida maana ni mke wake
Mungu Nje ya kutupa akili,alitupa utashi uwezo wa kupambanua mambo na kuyatatua, mtu anapokuwa Hana uwezo wa kupambanua mambo na kuyatatua maana yake Wenda hajitambui au uwezo wake wa uelewa mdogo,mara chache sana Huwa magonjwa ya akil
Mtoto anapolia tumaini lake Huwa mzazi wake na mzazi akimshika na kumkumbatia hupata faraja,na hiyo ndiyo Nguvu aliyoiweka Kwa Kila mtu aliyehai,ndio maana unakuta mtu anapata tatizo Kali akiwa pekeake unakuta baadaye taratibu anaanza kupoa Lile tatizo kubwa linaanza kutoweka na kuhisi faraja Wakati Fulani akiwa pekeake au Wenda Kuna mtu anakufariji
ulishawahi ona siku umepata tatizo kubwa halafu ukaumia sana halafu baada ya muda Licha upo pekeako unakuta Lile jambo linaanza kupoa na faraja inaanza taratibu kuja bila hata kufarijiwa na mtu?hiyo ni Nguvu ya Mungu mwenye kupitia roho
Watu ambao mara Nyinyi hawana Imani sana na Mungu Wakati Fulani ni ngumu sana kupata faraja hii wakiwa pekeyao Sababu Nguvu ya tumaini Katika akili yake iliyo katika Mungu inakuwa ndogo,ndo maana tatizo likimpata faraja yake Kwa mganga,wanajimu nk,ndio maana Baadhi ya wanasaikolojia wengine Baadhi ya mambo suluhisho lao Huwa hawaelewi hufika Mahali husema Bora kujiepusha ukiona unamtu anakuuzi Sasa utaepuka wangapi?njia Bora kutafuta njia za kukabili
kadri moyoni unavyojaza matumaini ya Mungu Moyo wako hujijenga katika matumaini ndio maana unakuta Wengi wakipitapita wanaimba nyimbo za dini,wanasikiliza mahubiri kwenye radio memory,furashi nk kitendo hicho huhisi Raha na furaha hata akiumwa unakuta Mungu wangu au ukimuombea unakuta moyoni anapata faraja hiyo yote Sababu ya Roho Ile ya Mungu inavyomfariji mtu,Hali kadhalika mtu mwenye matumaini katika mambo ya Dunia unakuta mara Kwa mara anapenda mizikimiziki ya wasanii,vituko,vichekesho kujipa Raha anapokuwa na sonona
KADILI UNAPOWEKA VIPAUMBELE VYA KAZI, BIASHARA,MAISHA MAZURI,PESA, FAHARI ZA DUNIA KATIKA MOYO WAKO HUJIKUTA MATUMAINI YAKO YANAKUWA MADOGO NA KUANZA KUPELEKESHWAPELEKESHWA NA MAMBO HAYO,
ikiwa inafika Mahali unaacha ibada kisa kazi,inafika Mahali unaacha maombi kisa elimu,inafika Mahali unaacha mikutano ya ibada kisa Pesa,inafika Mahali unaacha kusoma vitabu vya kiroho kisa kichwa kinamambo mengi ya maisha hakitulii kumtafakari Mungu Kwa siku maana yake upo kwenye athari za kupoteza Tumaini kama huna nguvu ya kujidhibiti haraka maisha Yako yatabaki kupelekeshwa na utajikuta maisha Yako hayana kabisa furaha
Fanya kazi Kwa bidii ila usifanye kazi kama mtumwa mpaka unajutia kazi,Pesa isikupelekeshe Wala elimu isikupelekeshe,Wala uchumba au ndoa isikupelekeshe mpaka unaacha ibada au mahusiano Yako na Mungu kisa vitu Hivyo au Mali maana yake tumaini lako la maisha litapotea zaidi
ulishawahi sikia mtu kajiua kafukuzwa kazi au chuo,mtu kajiua mchumba kamuacha au mpenzi wake kamsaliti maana yake tumaini Katika maisha yake lilipotea ila tumaini lilikuwa Lile lililomfanya ajiue
tumaini la maisha haya ni Mungu tu,ndio maana ukijikwaa Mungu wangu,ukiumwa au ukiwa kwenye matatizo wewe na Watu wote wanabaki wapole Ili Mungu akusaidie licha wanafanya jitihada zingine
kamwe usiruhusu maisha Yako kupelekeswa,Kuna Vijana wanapelekeshwa hawaoi wala hawaolewi Wakati uwezo wanao kisa ngoja ninue gari baadaye huanza kujuta Bora ningeoaga kipindi kile,Kuna Watu wanapelekeshwa na nguvu ya ajabu kwenye mapenzi mpaka wanaacha kabisa kumheshimu Mungu wao kisa tu mapenzi,kazi,elimu baadaye hujikuta wakijuta tu
JITAHIDI SANA KUTENGENEZA MINDSET YAKO YOTE HAYA YAPO MFANISI YUPO KUWENI NA KIASI KWA KILA JAMBO ILI TUMAINI LAKO MAISHANI LISITOWEKE.
ushauri Bure na Unaweza uliza Bure utapata Msaada wa awali kimawazo pale unapohisi upweke kupita kiasi na kupoteza mwelekeo halisi wa maisha.
Maoni