ARTHRITIS ni nini..??
Arthritis ni mjumuiko au muunganiko wa magonjwa tofauti tofauti yasiyopungua 100± yanayotokana na namna yoyote ya hitilafu katika maungio ya binaadamu ambayo husababisha maumivu na pengine kuvimba kwenye eneo hilo la maungio. Hivyo kwa ufupi, arthritis sio ugonjwa mmoja, ni mjumuiko wa zaidi ya magonjwa 100.
NINI HUUNDA MAUNGIO
Sehemu ya maungio ya binadamu imeundwa na vitu hivi.
LIGAMENTS
ndicho kitu kinachoshikilia mifupa hii miwili pamoja. Hii ni kama utepe wa plastiki au mpira unaonyumbuka uliozunguka eneo hilo kwa nje, ukikunja goti inanyumbuka na ukinyoosha mguu inarudi.
CARTILAGE
(gegedu); huu ni utando unaofunika eneo ambalo mifupa hugusana ili kuzuia mifupa hii isisuguane moja kwa moja. Utando huu ambao kwa kiswahili tunauita gegedu huyawezesha maungio hayo kufanya kazi kiulaini pasipo kusababisha maumivu.
CAPSULE
hiki ni kitu kinachofunika maungio haya kikizunguka pande zote. Ndani ya mfuko huu wa capsule kuna synovial fluid ambayo huzalishwa na synovial membrane.
SYNOVIAL FLUID ni ute wa kulainisha sehemu hiyo ya maungio na synovial membrane ni utando ulio kwenye kuta za ndani za capsule.
Ugonjwa wa arthritis unasababishwa na hitilafu yoyote katika sehemu hizo za maungio ya mifupa. Inaweza kuwa cartilage inalika, upungufu wa synovial fluid, maambukizi ya vijidudu katika moja ya maeneo hayo au mchanganyiko wa matatizo.
AINA KUU ZA UGONJWA WA ARTHRITIS
1. Osteoarthritis (OA)
2. Rheumatoid Arthritis
3. Gout
4. Infectious Arthritis (septic)
5. Juvenile rheumatoid Arthritis
Tutaangalia kila ugonjwa kwa wakati wake pamoja na tiba yake
Maoni