Je, Nini Sababu Ya Kukosa Damu Ya Hedhi?

Chanzo cha asili kabisa cha kukosa hedhi ni ujauzito, kunyonyesha, pamoja na kukoma hedhi baada ya kufikia umri wa kukoma. Kwa namna hiyo basi, hakuna haja ya kumuona daktari. 

Mwanamke anapokuwa anapata hedhi kwa mpangilio mzuri bila kubadirika, hii inamaanisha kwamba vifuko vya mayai(ovaries), tumbo la uzazi(uterus), tezi ya hypothalamus na pituitary vinafanya kazi vizuri. 

Kukosekana kwa hedhi kunaweza kuashiria tatizo la moja ya sehemu hizo za mwili, kunaweza kukawa na kudhoofika kwa njia ya uzazi. Mambo ya mtindo wa maisha, matatizo ya magonjwa ya afya, na baadhi ya madawa pia husababisha kukosa hedhi.  

Sababu zinazofanya kukosa vipindi vya hedhi ni pamoja na hizi zifuatazo:

1.Uzazi Wa Mpango

Baadhi ya madawa ya uzazi wa mpango yanaweza kusababisha kukosa hedhi kwa muda wa miezi mitatu au kukosa hedhi kabisa moja kwa moja.

Hali hii inaweza kutokea katika miezi michache ya awali unapoanza kutumia dawa za uzazi wa mpango. Baadhi ya njia za uzazi wa mpango, kama vile, vijiti, sindano au vidonge vinaweza kusababisha kukosa hedhi.

2.Mapungufu Ya Virutubishi

Utapia mlo unaweza kuathiri utendaji kazi wa tezi ya hypothalamus na pituitary, hali inayoweza kupelekea kukosa hedhi. 

3.Mwili Kuwa Mwembamba

Mwili kuwa mwembamba kunaweza pia kuzuia tezi ya hypothalamus na pituitary kushindwa kufanya kazi sawasawa. Hali hii inaweza kusababisha aina ya kukosa hedhi inayofahamika kama, “kukosa hedhi kutokana na tatizo la tezi ya hypothalamus(functional hypothalamic amenorrhea)”.  

4.Msongo Wa Mawazo

Msongo wa mawazo unaweza pia kuathiri viwango vya homoni mwilini mwako, na ni chanzo kingine cha kukosa hedhi kutokana na tatizo la tezi ya hypothalamus. Watu wenye aina hii ya kukosa hedhi pia wana hali kubwa ya msongo wa mawazo.

5.Mazoezi Mazito

Mazoezi mazito ndio kisababishi cha tatu cha kukosa hedhi kutokana na tatizo la tezi ya hypothalamus. Baadhi wanakadiria kwamba nusu ya wanawake wanaofanya mazoezi mara kwa mara hupatwa na matatizo makubwa ya uzazi.

6.Ulaji Mbaya

Unapokuwa na tabia ya kula vyakula vibaya, kama vile chips, pilau kw asana, kunaweza kusababisha vipindi vya hedhi kukoma. Hali hii ya kukosa hedhi kwa kawaida hutokana na upungufu wa lishe au mwili kuwa mwembamba. 

7.Mwili Kunenepa Sana

Mwili kunenepa kwa haraka Zaidi kunaweza kusababisha mvurugiko wa homoni(hormonal imbalance), ambao unaweza kupelekea kukosa hedhi kwa muda. 

8.Madawa Ya Matatizo Ya Ubongo

Baadhi ya madawa ya matatizo ya akili yanaweza kuathiri jinsi tezi ya hypothalamus na pituitary inavyofanya kazi. Kama tezi hizi hazizarishi viwango sahihi vya homoni, basi vipindi vya hedhi vya mwanamke vinaweza kukoma. 

9.Mvurugiko Wa Homoni

Mvurugiko wa homoni ni tatizo ambalo huathiri asilimia kubwa ya wanawake duniani leo. Mvurugiko wa homoni unaweza kusababisha dalili kama hizi zifuatazo:

👉. Vipindi vya hedhi kubadirikabadirika
👉. Kuota vinyweleo vingi au ndevu
👉. Kushindwa kupata mimba
👉. Mwili kuwa mnene
👉. Kutokwa na chunusi sana usoni

Mvurugiko wa homoni unaweza kusababisha mwanamke kuwa na kiwango kikubwa cha homoni za kiume(hyperandrogenemia). Wanawake wenye mvurugiko wa homoni inaonekana kwamba silimia 78% yao wana homoni za kiume. 
Kwahiyo homoni za wanaume zinaweza kuathiri mzunguko wa hedhi na kupelekea mwanamke kukosa hedhi. 

10.Mayai Kushindwa Kukomaa

Kushindwa kukomaa kwa mayai ni pale vifuko vya mayai vinapokoma kufanya kazi kwa usahihi kabla mwanamke hajafikisha umri wa miaka 40. Hali hii inaweza kupelekea kukosa hedhi. Hata hivyo, haifanani na hali ya kukoma hedhi kipindi cha awali, ambapo ni pale hedhi inapokoma kabisa.

MAJALIWA YA MWENYEZI MUNGU KESHO MAJALIWA TUTAONGEREA MASWARA YA UGUMBA KWA WANAUME WA KIZAZI CHA SASA 

WENGI HAWANA UWEZO WA KUTUNGISHA MIMBA MBEGU ZAO ZINA HITILAFU KESHO MAJALIWA



Maoni