HALI YA KUTOA SAUTI YA KUJAMBA UKENI WAKATI WA TENDO LA NDOA
Kutoa hewa mithili ya kujamba ukeni ni hali inayowakuta wanawake wakati wa kushiriki tendo la ndoa ama inaweza kumpata mwanamke muda wowote
Hi ni hali ambayo kitaalam inajulikana kama (vaginal flatulence)
Ni kitendo cha hewa kutoka ndani ya uke (Queef)
Kitendo hichi huwafanya wanawake kutojiamini au kujisikia vibaya pale wanapokuwa faragha na wenza wao
Huenda umewahi kujiuliza Je_ni Ugonjwa?
👉 Hapana hali hii sio Ugonjwa ni hali ya kawaida ambapo uke hutoa nje hewa ambayo imeingia ndani.
Wengi huuliza Eti kwanini hali hii hutokea hasa wakati wa wa tendo la ndoa?
👉Jibu ni kwamba wakati wa kushiriki tendo la ndoa hewa husukumwa ndani na uume hivyo kufanya ijae ndani na inapojaa hutoka kwa sauti hiyo kama ya kujamba, ni mfano wa pump inapojaza hew katika tube.
Kutokana na maumbile ya uke kwa ndani una mikunjo ambayo hairuhusu hewa kukaa hivyo husukuma nje hewa inayojaa pale tu inapoingia.
Mara nyinyi hewa hiyo inayotoka ukeni huwa haina harufu yoyote na ikitokea kuna harufu basi huenda mwanamke huyu ana maambukizi ukeni.
JE NINI HUPEKEKEA BAADHI YA WANAWAKE KUWA NA HALI HIYO NA WENGINE HAWANA?
Zipo baadhi ya sababu zinazopelekea uwe na tatizo hilo miongoni mwa sababu hizo ni;-
👇
👉Kulegea kwa misuli ya uke. misuli ya uke inapolegea huruhusu hewa nyingi kupita kwa kuwa uke unakuwa wazi sana yaani unatanuka.
👉Kunawa ukeni kwa kutumia maji moto.
Matumizi ya maji moto hufanya misuli ya uke Kulegea hivyo kuruhusu hewa kupita
_Pia matumizi ya maji moto yanaua bacteria walinzi ukeni hivyo ni rahisi kushambuliwa na maambukizi ya mara kwa mara ya fangasi kama kupata miwasho nk.
👉 Wanawake waliotoka kujifungua hukumbwa na hali hiyo kutokana na hali waliyopitia wakati wa kuzaa lakini baada ya muda misuli hurudi na kuwa sawa.
👉 Wakati mwingine Mikao au style zinazo tumika Wakati wa kushiriki tendo la Ndoa* huruhusu kwa urahisi hewa kuingia ukeni. Ni vema kama inatumika basi mwanaume asiwe anatoa uume wote nje na kuingiza tena kufanya hivyo anasukuma hewa ndani hivyo anaweza kufanya bila kutoa uume wote nje mara kwa Mara.
Kwahiyo Msijisikie aibu inapotokea Hali hii, Ni kawaida na Haina madhara!
Imarisha Afya $ Uzazi.
NIWAKATI WAKO SAHIHI WEWE MWANA MMKE UNISIKILIZE MAKINI *JINSI ya Kubana Misuli ya Uke Uliolegea
👇👇
✍️Mazoezi ya nyonga ni moja ya mazoezi mazuri zaidi katika kukaza misuli ya uke wako. Mazoezi haya yanalenga kuimarisha misuli ya kibofu cha mkojo, mkundu, utumbo mdogo na kizazi pia.
💄Misuli ya uke inapolegea utaanza kuona dalili kama👇👇
mkojo kutoka pasipo ridhaa yako
kujisikia haja ndogo kila mara
kupata maumivu eneo la nyonga
kujamba ukeni wakati wa tendo na
kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
Pamoja na kwamba mazoezi haya ya nyonga yatakusaidia kukaza misuli ya uke, siyo tiba kwa changamoto kubwa kama fistula, ambapo mwanamke anatokwa na haja ndogo na kubwa bila kujizuia. Fistula inatibika bure na wahitaji kufanyiwa upasuaji mdogo tu hospitali.
Mazoezi ya Kubana Misuli ya Uke ni pamoja na👇
🥏Zoezi la Kegel kubana misuli ya uke
Muda mzuri wa kufanya zoezi hili ni pale unapoenda haja ndogo. Wakati wa kukojoa ndipo unaweza kutumia misuli inayotakiwa. Kama utafanikiwa kubana misuli sahihi wakati unakojoa na ukagundua mabadiliko kwenye speed ya mkojo basi hapo umepatia zoezi.
👉Wakati unakojoa bana misuli ya ndani ya uke ili kuzuia mkojo usitoke. Bana mkojo wa sekunde 10 kisha uachie kwa sekunde kadhaa bana tena. Mwanzo utakuwa mgumu lakini usikate tamaa endelea kufanya mpaka upatie zoezi. Usifanye kila muda unapoenda kukojoa ila jitahidi ufanye mara 4 kwa siku.
👉Njia ingine ya kufanya zoezi la kegel
👇
Kama utashindwa kufanya zoezi wakati wa kukojoa basi unaweza kujaribu njia ingine kwa kuingiza kidole ukeni mpaka ndani na ujaribu kubana misuli ya uke uone kama kidole kinabanwa. Fanya zoezi hili awamu 5 kila unapokojoa au unapoingiza kidole. Na ufanye mara tano mpaka 10 kwa siku.
Kama ilivo kwa mazoezi mengine, unavofanya zaidi kila siku unapata uzoefu na ndivyo unazopatia zaidi.
✍️Pelvic Tilt Exercise ili Kubana Misuli ya Uke
👉👉Kukaza misuli ya uke wako kupitia zoezi hili fanya haya👇👇
simama wima na makalio yako yaegemee ukuta.
vuta tumbo kwa ndani. Unapofanya hivi mgongo wako utanyooka kuelekea kwenye ukuta
bana tumbo lako kwa muda wa sekunde 4 kisha jiachie
fanya hivi mara 10 na awamu tano kwa siku nzima.
👉👉 Hitimisho Kuhusu Kukaza Uke
Fahamu tu kwamba maumbile yanatofautiana kwa kila mwanamke . Kwahivo usijilinganishe na rafiki yako nawe ukataka kuwa kama yeye. Kama ukiona mabadiliko kwenye uke wako yanayokufanya usifurahie tendo la ndoa, nenda hospitali onana na daktari atakupa ushauri wa kina.
Hutakiwi kuvumilia maumivu wakati unafanya tendo eti ili tu umridhishe mme wako hapana. Matatizo mengi yanafanya uke kuwa mkavu yanaweza kutibika. Kama una mashaka na uke wako muone daktari mapema kupata suluhisho. Vinginevyo upo hatarini kwa kupata uvimbe usio julikana kwako
Maoni