UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA TIBA YAKE

UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA KIUME  NINI  CHANZO CHAKE

Upugufu wa nguvu za kiume hutokea kwa wanaume wa rika lolote hasa katika umri mkubwa, ni tatizo kubwa la kiafya ambalo husababisha mgonjwa kuathirika kisaikolojia, wenza kushindwa kufurahia tendo la ndoa, ugumba na kuvunjika kwa mahusiano au ndoa.

  • Matatizo maalumu yanayohusiana na upungufu wa nguvu za kiume ni pamoja na
Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, 
Kushindwa kusimamisha uume, 
Kuwahi kufika kileleni na 
Kuchelewa sana au kushindwa kabisa kufika kileleni.

  • Pamoja na kwamba wagonjwa wengi hukimbilia kwenye tiba za asili matatizo mengi kati ya haya yanafahamika na yanaweza kutibiwa kwa tiba za dawa za kisasa(modern medicine) na ushauri wa kisaikolojia hasa kwa kubaini na kutibu visababishi.

Husababishwa na nini ???
Upungufu wa homoni ya kiume, Testosterone ambayo huusika na kuleta hamu ya tendo, kutengeneza mbegu za kiume, kujenga misuli na kuota nywele za kiume kama ndevu.
Upungufu wa testosterone husababisha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa na mabadiriko ya tabia za kijinsia.

Magonjwa mbalimbali kama kisukari, Shinikizo la damu, magonjwa ya mishipa ya damu, Kiharusu/stroke, ajali ya uti wa mgongo na madhara ya upasuaji husababisha kushindwa kusimamisha uume kabla na kushindwa kuendelea kusimamisha uume wakati wa tendo la ndoa.

Matatizo ya Kisaikolojia kama Msongo wa mawazo, hofu, kujituhumu, kutojiamini, kufarakana kwa wenza, historia ya maumivu wakati wa tendo lililopita, matatizo ya kikazi/kipato pia husababisha kukosa hamu, kushindwa kuendelea kusimamisha uume, kufika kileleni haraka/kabla au mwanzoni wakati wa tendo la ndoa.

Upungufu wa nguvu za kiume pia unaweza kutokea ikiwa ni matokeo ya madhara ya dawa za kutibu magonjwa sugu, dawa za kutibu shinikizo la damu, baadhi ya dawa za kutibu magonjwa ya akili, pombe, sigara,dawa za kulevya, kutofanya mazoezi, uzito kupita kiasi na kula sana.

Kitendo cha shahawa kupanda kwenye kibofu cha mkojo badala ya kushuka na kuingia kwenye njia ya uzazi ya mwanamke hufahamika kitaalam kama Retrograde ejaculation, hutokea kwa baadhi ya wanaume wenye ugonjwa wa kisukari na waliofanyiwa upasuaji wa shingo ya kibofu cha mkojo au tezi dume, hali hii husababisha ugumba kwa wanaume kwa kiwango kikubwa.

Je utapenda kujua zaidi kuhusu matibabu ya tatizo hili au una tatizo lingine la kiafya ambalo utapenda kupata Elimu na Ushauri.

Niwakati wako sahihi upone 
Namna ipo na unaweza pona

Maoni