SIKU YA KUPATA UJAUZITO


SIKU YA KUPATA UJAUZITO























Mimba hutokea pindi mbegu ya kiume (sperm) inapokutana na yai la mwanamke (ova) na kuungana kwa pamoja kutengeneza selli moja iitwayo zygote. Seli hii hukuwa na kujakuwa mtoto kamili. Kawaida kitendo hiki hufanyika ndani ya masaa 12 toka yai kukomaa na kuletwa kwenye mirija ya falopian. Baada ya mimba kutungwa itabakia pale kwa masaa kama matatu, kisha huanza kusafirishwa na kupelekwa kwenye tumbo la mimba ambapo huku litabakia mpaka mtoto kuzaliwa.

Mwanamke hutoa yai moja kila mwezi kutoka katika ovari moja. Kuna wakati mwanamke huenda akatowa mayai zaidi ya moja, hali hii si kawaida. Yai hili linaweza kuwa hai ndani ya masaa 12 mpaka 24. hutokea pia likaweza kuwa hai mpaka masaa 48. ndani ya muda huu yai ni lazima likutane na mbegu ya kiume ili mimba itungwe. Kipindi hiki kitaalamu kinajulikana kama fertile window.

Mbegu ya mwanaume huweza kudumu kuwa hai ndani ya siku 5, ndani ya siku hizi mbegu hizi huwa zipo hai hivyo zinaweza kurutubisha yai. Mwanaume huto zaidi ya mbegu milioni 300 ejaculation moja. Katika mbegi hizi mbegu moja ndio hutakiwa kuungana na yai.

Siku za mwanamke kuweza kuwa kati ya 21 mpaka 35 inategeme na mwanamke. Kikawaida walio wengi siku zao ni 28. katika siku hizi zipo siku 6 tu ambazo mwanamke anaweza kupata ujauzito. Siku hizi huanzia siku ya 11,12,13,14,15 na 16. katika siku hizi siku ya 14 ndio ambayo huaminika zaidi kuwa yai hutolewa ziku hii. Ni vyema kukutana kimwili katika siku hizi kwa wanaotafuta ujauzito. Sio lazima pia kufululiza inawezekana kuruka ila nivyema kutoikosa siku ya 13 na 14.

Pia kuna dalili kadha za kuijua siku hii kama kuzidi kwa joto la mwanamke siku moja kabla na siku ile ya kutolewa kwa yai. Pia kuongezeka kwa utelezi kwenye shingo ya uzazi. Pia mwanamke anapenda sana kukutana kimwili kukaribia siku hii. Vipo vifaa pia vya kuitambua siku hii. Siku hizi huhesabiwa kutoka kupata hedhi na kuendelea. Pia siku hisi kutofautiana kwa wanawake.


SIKU YA KUPATA UJAUZITO
Kawaida wanawake walio wengi mzunguruko wa siku zao ni siku 28 lakini wapo ambao ni zaidi ya hapo na wapo ambao ni chini ya hapo. Sasa ni ipi sikuya kutolewa kwa yai kwa wanawake hawa?. makala ya hapo juu katu haikugusa kipengele hiki.

Kikawaida yai hutolewa (ovulation) kwa makadiria ya siku 12 mpaka 16 kabla ya kupata hedhi nyingine. Yaani unaweza kuhesabu kabla ya kuingia hedhi siku 12 nyuma, kisha toa siku 4 mnyuma ndani ya siku nne zizi ndizo yai hutolewa. siku hizi ndizo moja wapo yai hutolewa. Kwa mfano:--

1.Mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21, sasa tunatoa siku 12 nyuma kabla ya kuingia hedhi (21 - 12 = 9) kisha toa nne nyuma (9-4=5) basi mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 5 na 9 katika siku zake.

2.Mwanamke mwenye mzunguruko wa siku 32: tunaanza kutoa siku 12 nyuma kabla ya kupata hedhi yake (32-12=20) tonatoa siku nne tena nyuma (20-4=16) kwa hiyo mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 16 mpaka 20


Maoni