UVIMBE KWENYE KIZAZI (FIBROIDS)

 UVIMBE KWENYE KIZAZI (FIBROIDS)

Fibroids ni nini?
Fibroids ni uvimbe usio wa saratani ambao hujitokeza kwenye kuta za mfuko wa mimba,uitwao uterusi, uvimbe huu husababisha kubadilika kwa shape na size ya kizazi na pia dalili zingine mbaya. Wanawake wengi huanza kupata maumivu makali wakati wa hedhi kutokana na uwepo wa uvimbe kwenye kizazi(fibroids) .



DALILI ZA UVIMBE KWENYE KIZAZI (FIBROIDS)

  • •Kupata Hedhi inayochukua siku nyingi kuanzia 7 na zaidi.
  • •Hedhi nzito.
  • •Kujisikia umeshiba mda mwingi
  • •Maumivu ya nyonga.
  • •Kupata mkojo mara kwa mara na kushindwa kutoa mkojo wote kwenye kibofu.
  • •Kupata maumivu wakati watendo la ndoa.
  • •Maumivu chini ya mgongo na kwenye miguu.
  • •Madhara mablimbali ya uzazi kama ugumba na mimba Kuharibika .

AINA ZA UVIMBE KWENYE KIZAZI - ( FIBROIDS ).

Jina la kitabibu la fibroids ni leiomyoma au myoma
Ukubwa, mahali ulipo uvimbe na pia idadi ya vimbe hizi inachangia zaidi kwenye uwepo wa dalili mbaya aatakazopata mwanamke.
Inawezekana kabisa kuwa na aina zaidi ya moja ya fibroid katika muda mmoja kama zitatokea mahali tofauti tofauti kwenye uzazi wa mwanamke.




Aina kuu za uvimbe kwenye kizazi(fibroids) ni kama zifuatazo

INTRAMURAL FIBROIDS
Hii ni aina marrufu zaidi na zinawatokea zaid wanakwake. Aina hii ya fibroid hukua na kumea kwenye misuli ya ukuta wa uterus. Kadiri zinavokua basi husababisha kupanuka au kuvutika kwa kizazi na kusababisha dalili kama hedhi ya muda mrefu inayoambatana na maumivu ya nyonga.

SUBSEROSAL FIBROIDS
aina hii ya fibroids hukua nje ya ukuta wa mfuko wa mimba, wakati mwingine kuelekea kwenye kibofu cha mkojo. Aina hii ya fibroids huweza kusababisha maumivu ya chi ya mgongo kutokana na kwamba uvimbe huu unasukuma nerve za sipnal na kusababisha presha kubwa kwenye eneo la chini ya mgongo.

SUBMUCOSAL FIBROID
Saina hii ya fibroid hukua karibu na ukuta wa Uterus na inaweza kusababisha bleed ya muda mrefu na shida kwenye kushika ujauzito.

CERVICAL FIBOIDS
Hizi hukua kwenye tishu za mlango wa kizazi ambao huitwa Cervix , Hutokea mara chache sana ukilinganisha na aina zingine za fibroids.

NINI KINASABABISHA MWANAMKE KUPATA FIBROIDS

  • kama mama au dada yako aliwahi kuugua tatizo hili basi wewe pia utakuwa kwenye hatari zaidi ya kupata uvimbe huu.
  • Umri: uvimbe kwenye kizazi (fibroids) hutokea zaidi kwa wanawake wanaokaribia kukoma hedhi kuanzia miaka 35 mpaka 40.
  • Lishe: matumizi ya vyakula vya wanga na sukari kupita kiasi huongeza hatari ya kupata fibroids.
  • Uzito mkubwa na kitambi: wanawake wenye uzito mkubwa na kitambi wako kwenye hatari zaidi ya kupata fibroids .
  • Wanawake wenye shinikio kubwa la damu.
  • Matumizi ya njia za kupanga uzazi: kama vidonge huongeza ukuaji wa fibroids kwani vidonge hivi huweza kupandisha homoni ya estrogen kwa wingi.
  • Kubalehe mapema: wanawake wanaobalehe mapema na kuanza kupata hedhi chini ya miaka 10 wako kwenye hatari zaidi ya kuugua fibroids

Maoni