UJASIRIAMALILI
Mjasiriamali ni mtu mwenye uthubutu, asiyeogopa kushindwana mwenye maamuzi binafsi ambaye ameamua kuingia kufanyakazi halali inayomuingizia kipato chake binafsi kwa kutumiaujuzi wake, fedha zake, utaalamu wake n.k. Ni mtu mwenye upeowa kuona nafasi (fursa) haraka na kuitumia. Huyu mara zotehufananishwa na mchezaji ambaye hapotezi nafasi anayoipata.Kifupi ni mtu wa maamuzi na uthubutu bila kusubiri.Mtu huyu hana tabia ya kugeuka nyuma na kuangalia alipotoka,au nini watu wanasema kumkatisha tamaa, lakini yeye huangaliakesho yake itakavyokuwa nzuri, kuliko leo yake ambayo watuwanambeza na kumkatisha tamaa juu ya wazo alilonalo.Sifa za mjasiriamaliMjasiriamali huwa ana sifa za kipekee zinazomtofautisha namwingine. Habari njema ni kuwa sifa hizi hatuzaliwi nazo. Sifahizi tunazitengeneza wenyewe kwa kwa kujifunza kupitia vyanzombalimbali.Zifuatazo ni baadhi ya sifa za Mjasiriamali;

1. Mjasiriamali ni kiongozi
Walimu wengi wamekuwa hawafundishi hii kama sifa yamjasiriamali lakini hii ni moja ya sifa muhimu anayopaswa kuwanayo mjasiriamali. Mjasiriamali kwanza lazima awe kiongozi wamaisha yake. Ajue kujisimamia mwenyewe na kusimamia mamboyake yeye kama yeye bila kusubiri mtu kutoka nje. Mjasiriamalini lazima ajue kuiongoza biashara yake lakini hasa kuwaongozawatu anaofanya nao kazi kama wapo.2. Mjasiriamali ni mwenye uwezo wa kufanya maamuzibinafsiMtu yeyote mwenye sifa ya kuwa mjasiriamali ni lazima awena sifa hii ya kuwa na maamuzi katika maeneo mbalimbali hasa Mwongozo wa Biasharamaamuzi juu ya jambo fulani ambalo analiona kwake lina faida.Ni mtu asiyechelea kutumia kila fursa anayoiona.3. Mjasiriamali ni mtu mwenye bidii (Anayejituma)Mjasiriamali ni lazima awe ni mtu anayejituma na ambayeameachana kabisa na tabia ya uvivu. Kwake yeye kufanya kazikwa bidii ni sehemu ya maisha yake na anafahamu vyema kuwakama akilala hata ujasiriamali wake utalala pia.4. Mjasiriamali ni mtu asiyekata tamaaNi lazima mjasiriamali yeyote awe na moyo wa kutokata tamaahata kama anapitia katika changamoto gani. Ni mtu anayeangaliambele tu na hata hafikirii juu ya changamoto na maneno yakukukatisha tamaa ya watu. Kwake yeye changamoto humpakujifunza na kuendelea kuwa bora kwa kila anachokifanya.5. Mjasiriamali ni mtu anayetumia kile alichonachomkononiMjasiriamali ni lazima awe mtu wa kutumia kile alichonachomkononi. Mjasiriamali huwa hasubiri mtaji wa laki moja wakatiana elfu thelathini mkononi. Hufikiri namna ya kutumia elfuthelathini wakati akisubiri mtaji wa shillingi elfu hamsini.6. Mjasiriamali ni mwenye kiu ya ndani ya kufanikiwaMjasiriamali ni lazima awe na msukumo wa ndani wa kuonakuwa atafanikiwa kwa chochote anachokifanya. Msukumohuu ndio humfanya kuamka mapema na kufanya vile anawezakufanya bila kuangalia wanaomkatisha tamaa.7. Mjasiriamali ni mbunifuMjasirimali ni lazima aweza kufanya kwa utofauti na kuleta vituvipya ili kuongeza tija katika kile anachokifanya. Mjasiriamali nilazima awe na uwezo wa kujiongeza na kuonesha utofauti katikakile anachokifanya.8. Mjasiriamali ni mgunduziMjasiriamali ni mtu anayepaswa kufanya vitu vipya ambavyohavijawahi kutokea. Ni mtu anayetumia muda mwingi kutafutavitu ambavyo havijawahi kutokeaHIVI NI BAADHI MINGONI MWA VITU UNAVYOTAKIWA KUFAHAMU KUHUSU UJASIRIAMALI.
Maoni