NAMNA MWANAUME  AMBAYE ANA TATIZO LA UDHAIFU WA MBEGU ZAKE, AWEZE KUWA NA UWEZO WA KUKUPA UJAUZITO.

Suala la kupata mtoto katika familia  haliegemei upande wa kina mama tu.

Mimba kutunga ni matokeo yanayotegemea upande wa kike na wa kiume japokuwa kwa jamii zetu tumezoea kuwa familia ikikosa mtoto basi lawama huenda moja kwa moja kwa mwanamke kuwa yeye ndiye chanzo cha tatizo jambo ambalo huwa sio la kweli mpaka wote kwanza mfanye vipimo kubaini nani haswa ni chanzo iwapo kama ndoa imedumu muda mrefu bila kupata mtoto.

Leo nitakuelekeza njia asili ambayo imekuwa ikitoa uhakika wa kuponesha tatizo la mwanaume kuwa na shida ya manii / mbegu zake kushindwa kumpa mimba mwanamke kwa sababu ya uchache au udhaifu wake.




 Majani Ya Mpera
Majani ya mpera ni utafiti unaoonyesha kutibu tatizo la ugumba kwa mwanaume, naomba unielewe hapa, majani haya hayaongezi nguvu za kiume ila yanasaidia kwa mwanaume mwenye tatizo la kushindwa kumpa mimba mwanamke kwa sababu ya udhaifu wa manii yake.

Madhaifu ya mbegu za mwanaume tunayoyasemea ni kama 

1.Oligospermia-hii ni hali ya kupungua kwa mbegu za kiume
2.Aspermia =hii ni hali ya kutokuwa na majimaji yaani(semeni) ambayo husaidia kusafirisha mbegu za kiume
3.Azoospermia-ukosefu wa mbegu za kiume 
4.Teratospermia- hii ni hali ya kuongezeka kwa mbegu za kiume ambazo hazijakamilika yaan hazina either kichwa au mikia
5.Asthenozoospermia hii ni hali ya mbegu za kiume kushindwa kujongea (kuogelea au kusafiri) kuelekea ndani ya via vya uzazi wa mwanamke ili kuweza kurutubisha yai la mwanamke

KUONGEZA WINGI, UBORA WA MANII na NGUVU ZA KIUME.

Ni rahisi kugundua madhaifu ya mwanaume kwa kuangalia baadhi ya vitu....
Mwanaume dhaifu shahawa zake huwa nyepesi, na zikiingia ukeni huwahi kutoka nje, rangi ya shahawa zao huwa ni nyeupe sana kama uji wa sembe, na hata ukizivuta zinawahi kukatika bila kufikia sentimita 2

NAMNA YA KUANDAA DAWA

1: Chuma majani teketeke ya mpera, namaanisha yale majani machanga kabisa (usichukue majani ambayo yamekomaa), chuma kiasi cha bakuli.
2: Yasage au yatwange mpaka yalaike vizuri
3: Chukua dawa yako, uchanganye na maji lita moja uchemshe kwa dakika tano tu, ipua.
4: Ikishapoa utaichuja na kumpa mume glass moja anywe asubuhi mchana na jioni au unaweza kufanya asubuhi na jioni pekee km ni mtu wa kazi mchana.

Ukifululiza kwa siku saba mwenye utaona mabadiliko maana utamuona akiwa na uhitaji wa kufanya mapenzi bila hata kumlazimisha maana wingi wa mbegu zake unamfanya awe na uhitaji wa kufanya tendo la ndoa na hata umwagaji wa shahawa utauhisi tu maana manii yanakuwa mengi halafu mazito.

Mbinu za ziada za kufanikisha zoezi la mwanaume kuwa na uhakika wa kutungisha mimba ni kumpa likizo ya siku walau 7 bila kufanya mapenzi

Kumpa muda mrefu bila kufanya mapenzi husaidia korodani zake kuzalisha manii mengi na yenye bora kwa ajili ya kurutubisha yai la mwanamke.

Mfano tuseme una mzunguko wa siku zako ni siku 28 kwa maana siku zako za kubeba mimba ni kuanzia siku ya 11 hadi 15. Mume mpe likizo kuanzia siku ya tano, uje ukutane naye siku ya 12

Upande wa vyakula vizuri kwa ajili ya manii ya mwanaume kulingana na mazingira yetu ya Kitanzania ni vyakula visivyokobolewa kama ugali dona, mihogo, viazi n.k huku mboga na matunda ikiwa ni samaki wabichi, bamia, ndizi mbivu, karanga, tikiti, mbegu za maboga, komamanga, parachichi, asali mbichi na mboga za majani. Kama mwanaume atapata walau viwili hadi vitatu kwenye hiyo orodha kwa wingi wa kutosha hakika anajiweka katika nafasi nzuri ya kuwa na manii bora + nguvu za kiume kwa ujumla.
Mshauri aache pombe, sigara na vilevi kama ni mpenzi wa vitu hivyo.

WANAUME WENGINE HUWA NA MATATIZO MOJA KWA MOJA YA UPUNGUFU NGUVU ZA KIUME 

yaani unakuta mwanaume kufika kileleni dakika 1 na kurudia hawezi au mpaka akae muda mrefu, uume wake unasimama legelege au akifika kileleni anatoa manii hata kijiko hakijai sometimes anafika kileleni bila kumwaga chochote. Wanaume wa hivi sio wa kuchekwa au kudharauliwa, hii ni hali inayowapa stress sana na wana hangaika sana kutafuta msaada hivyo kama unae mume na ana matatizo hayo basi onesha ushirikiano wa kumuonesha njia hii ya asili nayokuandikia

Maandalizi
Mahitaji ni Asali mbichi ya nyuki wadogo lita 1, tangawizi kubwa nne au sita [osha, menya kisha katakata vipande], vitunguu saumu ujazo wa glass moja [menya vizuri kuondoa maganda yake], unga wa msamitu vijiko nane, unga wa mdalasini vijiko sita mpaka nane, unga wa habat sawda [black seed] vijiko vinne mpaka sita.

Jinsi Ya Kuandaa
1.  Chukua tangawizi zako na vitunguu saumu uweke kwenye blenda kisha usage mpaka vyote viwe laini.
2. Weka unga wa msamitu, mdalasini na unga wa habat sawda kwenye blenda kisha taratibu huku ukiwa umewasha blenda mimina taratibu asali mbichi ya nyuki wadogo mpaka lita nzima iishe kwa muda wa kama dakika mbili juisi yako itakuwa tayari.
3. Zima blenda na uweke juisi yako kwenye kifungashio safi ikae kwa masaa 6 

ITAKUWA TAYARI KWA MATUMIZI

MATUMIZI YA DAWA
Mwanaume atakuwa akilamba/kula vijiko viwili asubuhi kabla ya kula chochote, na usiku tena vijiko vitatu kabla ya kulala

kama mwaume ana tatizo la uzito mkubwa au anataka kukata kitambi, hiyo juis ya nguvu za kiume ataitumia kwa kuchukua vijiko vitatu na kuweka kwenye glass ya maji kisha kukamulia kipande cha limau na kunywa.

Nikukumbushe kwamba hii tiba ya jumla ni kwa ajili ya changamoto zote za kukosa nguvu za kiume
Kuanzia kwenye kuongeza wingi na ubora wa manii, kuondoa athari zilizotokana na upigaji punyeto na kuongeza kiwango cha msisimko wa tendo la ndoa.

#ASMOH

Maoni